Ya Hussei Bashe Yafichuka, Nani alimuua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Hussei Bashe Yafichuka, Nani alimuua?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Sep 13, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Lile sakata la kada wa chama cha mapinduzi (CCM) Hussei Bashe kuenguliwa katika nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo la Nzega mkoani Tabora kwa kisingizio kuwa si raia ,limechukua sura Mpya baada ya waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Lawrence Masha ,sasa kaandika barua rasmi kusisitiza kuwa ni rahia halali
  Kwa mujibu wa barua hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho "'yah: upotoshwaji juu ya uraia wa wako:Masha anamuandikia Bashe akisisitiza juu ya uhalali wa uraia wake huku nakala zikipelekwa kwa katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba na katibu Mkuu ,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  Barua hiyo yenye kumbukumbu namba SAB.27/75/01/18, Masha alisisitiza kuwa tamko la uhalali wa uraia wa Bashe ,uliwahi kuthibitishwa katika barua ya wizara yake yenye kumbu kumbu namba DN 109758 ya Agosti mwaka huu,iliyoandikwa kupitia Idara ya Uhamiaji.
  '' Kwa mara nyingine nachukua fursa hii kuthibitisha kwa mujibu wa kifungu namba 5(1) au 7(8)cha sheria ya urahia namba 7 ya mwaka 1995 wewe ni raia wa Tanzania wa kuzaliwa"Alisema
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Huyu Masha vipi mbona hakuyaeleza hayo kwa mgombea mwenzie wa nyamagana kwa tiketi ya Chadema?
   
 3. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  May be rizione kk
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Uchaguzi uchaguzi
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ridhiwan ndo mkamponza bashe baada ya kumlazimisha baba ake wamuondoe kijana huyu, CCM sasa ni kama muungano wa familia, a dead operarating political party.
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  ridhiwani na beno malisa wanaua umoja wa vijana ccm vijana shtukeni mjiunge chadema otherwise u r all finished
   
 7. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni stupidity ya kikwete kuto kuwa na akilk ya kumuwezesha kusoma Alana za nyakati.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mwalimu alikuwa sahihi kutoiingiza familia yake kwenye siasa.
   
 9. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Hili masha nalo jehu tu...

  Aandike nyingine kwa mpinzani wake wa Nyamagana....

  Masha... "If you can't beat them, join them"
   
 10. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  acha uchizi baba askofu hakuna waziri bora kwa karne hii kama Masha na tanzania inajivunia sana kijana wetu Lowrence endelea kutikisa nyamagana baba,,wawecha wawecha sana
   
 11. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  CCM inatia kichefuchefu kila mtu yeye ni mkubwa yeye ndie mwenye mamlaka :mad2::mad2::mad2::mad2::mad2: Masha, Makamba, Rizimoja wameyakoroga ss wanaanza kuyanywa moja baada ya mwingine. Kaanza Masha wengine watafuatia
   
 12. K

  Keil JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CCM imejaa wasanii na wahuni. Masha alipoitwa kuja kushughulikia swala la Bashe, alipoulizwa kuhusu swala hilo, aliwajibu waandishi wa habari kwamba swala la uraia wa Bashe halina utata. Walipotaka afanunue alimaanisha nini, alikwepa swali na kurudia kusema swala hilo halina utata. Hapo aliwaacha solemba waandishi wakiwa hawajui kwamba Masha anakubaliana na CCM au anakubaliana Idara ya Uhamiaji?

  Ninashangaa kusoma barua hiyo akisema kwamba Bashe ni Raia halali wa Tanzania. Kwanini hakutoa firm statement kama hiyo tangu siku ya kwanza alipoulizwa?

  Conclusion ni moja, Kikwete, Kamati ya Maadili, CC na Masha mwenyewe, wote walijua nini kilikuwa kinaendelea. Kwa kifupi Bashe hakuwa anatakiwa na ili kummaliza kabisa, makatibu wote wa matawi waliokuwa wanamuunga mkono wakati wa kura za maoni, some of them wamehamishwa na wengine kutishiwa kwamba Kigwangala asiposhinda watashughulikiwa.

  On the other hand, Bashe mwenyewe ameishaanza kusukuma tuhuma kwa viongozi wake wa Mkoa kwamba ndo walimpikia majungu. Lakini hajui hizo tuhuma zilizopikwa zilianzia wapi au malengo yake yalikuwa ni nini. Inawezekana anaweza kuwa anakwepa more msuguano na UVCCM, Riz1, na Mkulu. Sasa ili abaki salama inabidi atafute mchawi mwingine, maana hawa waliomroga (Riz1 na Malisa) hana ubavu nao na amegundua kwamba alicheza na moto, na akiendelea kucheza nao utamuunguza zaidi na kummaliza kabisa.

  Hata kama atabaki CCM bado hawezi kuwa na nguvu kama aliyokuwa amejikusanyia, ataanza kuogopwa na hivi amejiweka mbali na Kampeni ndio anajipalia makaa zaidi. Aangalie ustaraab wa kujiunga na chama kingine, vinginevyo ndoto ya una siasa ndo inaweza kuwa imeota mbawa.

  Ndiyo CCM hiyo bana .... ina wenyewe!
   
 13. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  BIRDS OF THE SAME FEATHER..... Utawajua kwa matendo yao...
   
 14. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #14
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni laana ya CCM kutokana na dhambi ya ufisadi. Sasa wanafisidiana wao kwa wao ktk chama!
   
 15. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kilichomponza Bashe ni kukubali kwake kuwa sehemu ya kundi la akina RA na El ambalo linajaribu kujifua ili kuweka mapandikizi yake katika kila maeneo nyeti ili kujenga mazingira ya kufanikisha azma ya kumtakasa mheshimiwa wao ili akubalike kuwa mgombea urais 2015. Lakini bila kujijua wanajikaanga kwa kula ganzi kwao katika kufanikisha kampeni za ccm mwaka huu..... Na bado kushughulikiwa mapandikizi yaliyopenyezwa Kawe na Ubungo
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Sep 14, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  ........You must be kidding!!!!!!
   
 17. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  You must be joking!!
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa mipumba kama wewe...wawecha wawecha kitu gani hujui unacho kiongea...
   
 19. K

  Keil JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kama wangemshughulikia na Peter Serukamba ningeamini kwamba kuna huo mpango. Bashe amemalizwa na Riz1 na haswa alipojibanza kwa Masauni.

  Kuna watu wanasema hata Kigwangala nae yuko kwenye kambi hiyo hiyo ya EL na RA. Kama wote walikuwa kwenye kambi ya EL na RA, kwanini wamchukue huyo Kigwangala na wamuache Bashe?

  Bado siamini kama JK anaweza kuwashughulikia EL na RA. Alishashindwa kwa kuwa jamaa wanatumia kama remote control na ndio maana akisikia EPA tu ana-panic, akisikia hoja za ufisadi ana-panic na wala hajaongelea lolote kuhusu ufisadi, ni wapambe wake tu ndio wanamsemea.

  Pia wagombea wote wenye nia ya 2015 hakuna ambaye niomeona anaongozana na Mkulu kwenye Kampeni. Mzee wa Joka la Mdimu alipita bila kupingwa lakini haonekani popote, Prof alionekana Mby tu, baada ya hapo kapotea. EL na RA hawajaonekana, labda wanasubiri JK akienda mikoani kwao.

  Kama JK angekuwa anawadhibiti EL na RA, wala asingekubali akina Muhingo Rweyemamu wawe wanasimamia Press ya Kikwete. Muhingo ni mwajiriwa wa RA, na bado hata Salva yuko loyal kwa RA kuliko kwa JK. Kama kweli Kikwete alikuwa ana nia ya kujinasua kutoka kwao angeachana na akina Rweyemamu (Salva na Muhingo) na bado kuna watu wengi sana wa EL na RA ambao wako kwenye timu ya Kikwete. So kusema kwamba EL na RA watashughulikiwa uchaguzi ukiisha, hiyo ni ndoto. Sana sana tusubiri maajabu kama hamjasikia EL ni Minister au Prime Minister kabisa.
   
Loading...