Ya Gazeti la Raiamwema na makala za Mbwambo; Tujadili hoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Gazeti la Raiamwema na makala za Mbwambo; Tujadili hoja

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tafakari, Oct 8, 2010.

 1. T

  Tafakari New Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gazeti hili na hasa makala ya Johson Mbwambo ni za chuki za wazi kwa JK imekuwa ada kwa makala za Mbwambo kila wiki kumsema,kukejeli na kumkosoa vibaya JK.kwa muda mrefu sana hali hii inatia kinyaa na kumuona Mbwambo ni mtu asiyeaminika.Tukumbuke kuwa kabla ya kampeni za uchaguzi mtu huyu aliandika makala huku akisema kuwa Waandishi wazingatie maadili katika kipindi hiki.
  Lakini mlolongo wa makala zake toka mwanzo wa kampeni umeanza kwenda kinyume na kile alichokiandika kabla ya kampeni.Umeanza kuonyesha kuwa Mbwambo amekuwa na agenda yake iliyojificha dhidi ya JK.Mara aseme kimfaacho Jk ni asasi na si urais huku akisahau kuwa ni Kikwete huyu huyu ambaye amekuwa madrakani kwa miaka mitano iliyopita huku Mbwambo akiwa kama mwananchi wake. Hili ameliandika katika makala yake ya jana 06/10/2010.Amefikia mahali akathubutu hata kuandika kuwa inafaa JK akajifunze kwa Rais Kagame wa Rwanda.Sina hakika kama alitaka JK akajifunza kutumia nchi za wengine kufadhili ghasia na kutumia nafasi hiyo kusaidia nchi yake au alimaanisha JK akajifunze jinsi ya kuwanyima wapinzani uhuru na kutishia vyombo vya habari,sijui hasa alimaanisha nini.Labda Watanzania wenzangu mtanisaidia.
  Hivi Ukubwa wa Tanzania utaufananisha na Rwanda? kama kujifunza kwanini Kagame wa Rwanda asije kujifunza kwa JK KWENYE ujenzi wa Chuo kikuu cha kuigwa cha Dodoma?Mbwambo hivi Rwanda wana chuo kama UDOM? umeshindwa kumpa heko JK hata kwa jambo kama hilo?Au wewe ndo ulipanga shughuli hiyo?Maandishi ya MBWAMBO hayana tofauti na mwandishi anayetumia jina la bandia anayejiita MSOMAJI RAIA hawa ni kama mapacha na Mbwambo kuanzia mtiririko wa uandishi wao,mawazo hasi dhidi ya JK, chuki zao za wazi zisizo na sababu kwa JK .HUYU MSOMAJI RAIA kaanza kuandika toka mwaka jana kuwa Rais Jk hashauriki. Hiyo ilikuwa mwezi wa tisa 2009. mwaka huu kajisahau kaandika kuwa Rais Kikwete anasikiliza marafiki zake sana. sasa mtu ambaye hashauriki atasikiliza marafiki na watu wake wa karibu?Cha ajabu minal rahman Mbambo kawahi kuandika makala kumsifu waziri Mkuu Mizengo Pinda kama waziri makini na mtendaji ni swali je aliyemteua Pinda si ndio JK? kazi hizo zinazo mfurahisha Mbwambo ndizo za JK.anafanya kwa maelekezo ya JK. HII NI DOUBLE STANDARDS.MFANO gazeti la jumatano ya jana Mbwambo karudia habari ya World Economic Forums uliofanyika Dsm 5-7 Mei 2010.
  huko nyuma aliwahi kuandika makala ya kukebehi mkutano ule kwa vile tu mgeni Rasmi alikuwa JK.imekuwa kama Mbwambo ana allergy na jina la JK.ameamua kuwa anarudia rudia maneno ya kumchafua JK.NAJIULIZA kama Mbwambo angepewa fursa ya kuambiwa ukimuombea jambo jema moja jirani basi wewe utapata mara mbili, yaani kama ukiomba jirani awe na nyumba basi Mwenyezi Mungu atakupa nyumba mbili. kwa Mbwambo angeomba yeye atolewe jicho moja ili Jk akose macho mawili.masikini maombi huombwa kwenye mambo mema tu.
  Napata ugumu kujua kama Raia mwema ni gazeti la Kina Ulimwengu au ni la Padri Slaa? maana Tanzania Daima inajulikana ni la Mbowe na hili ni la Slaa?
  Naishia hapa kwa sasa.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dear GOD, may you listen to our prayers and help us win this election (Chadema). Dear GOD, We ask now to ignore our enemies prayers.. Amen.
   
 3. K

  Kwanini Senior Member

  #3
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 121
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dREAMS.
   
 4. tempo_user1

  tempo_user1 Senior Member

  #4
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani kumwandika kwa namna ya kumkosoa ubovu wa JK ndio kukiuka maadili ya uandishi? Au bado uko katika zama zile za 'zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm?' Tafakari
   
 5. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hauna jipya, na mwenyezi mungu akulaani kwa mitizamo yako hiyo ya kifisadi!!!!!!!!!, I mean ULAAAANIWE NA AIDHA UFUNGWE KABISA WEWE FISADIIIIIIIIIIIIIIIII!!!, watu sasa maslahi ya nchi yapo mbele si CHAMA wala GAZETI, Ni kiongozi aliye na mwelekeo wa kutuondoa hapa tulipo!
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ccm woote mmejaa mawazo mdebwedo
  [​IMG]
   
 7. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hebu tuondolee takataka zako hapa, Huyo mwandishi ameongea ukweli mtupu.Nahisi wewe ni Mharilili wa gazeti la Mtanzania lililo kosa wateja na kuanza kugawiwa bureeeeeeee,
   
 8. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu Tafakari naomba nikuulize hivi yule Mhariri wa Daily News alitahariri nini vile ukurasa wa kwanza wa gazeti LETU kuhusu matokeo ya Uchaguzi?
   
 9. NAWAPASULIA

  NAWAPASULIA Member

  #9
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Tafakari nimesoma kwa makini makala yako nimesoma kila neno naona umejieleza vizuri bila shaka labda nikwambie watu wa aina ya Jonson Mbwambo ni wa aina gani, hawa ni watu wasio na shukrani kabisa.............kama unabisha nenda pale Mzumbe sekondari halafu uliza habari zake au tafuta file lake utaona alivyozoea kutukanatukana, kwanza huwa hawezi kujadili kwa hoja wala mantiki badala yake hujikita kwenye upande mmoja tu na kujadili kwa chuki labda niunge mkono wazo lako kwamba kama vile mtu anavyoweza kuwa na allergy na samaki basi na huyu Johnson Mbwambo ana allergy na Kikwete dawa ni kumpuuza kwa maana asiyejua maana haambiwi maana.
   
 10. H

  Hans20 New Member

  #10
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Who's Mbwambo?
   
 11. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,276
  Trophy Points: 280
  We nawe vipi? Inakuwaje unalihusisha gazeti zima na Dr. Slaa kwa vile tu makala moja imechambua udhaifu, ujuha na uzembe wa Bwana Kikwete? are you serious anyway au umetumwa wewe? - hii ni post yako ya tatu
   
 12. L

  Laurao New Member

  #12
  Oct 8, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbwambo?????!!!!!!!!!!
   
 13. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  None sense
   
 14. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,785
  Likes Received: 6,276
  Trophy Points: 280
  Rwanda wameendelea kwa KILA KITU as compared na TZ. Bwana JK atajifunza vitu vingi mno, ikiwamo utawala bora na jinsi ya kuwadhibiti wezi, manyang'au na mafisadi pamoja na kuweka vipaumbele vya serikali na kuvisimamia ipasavyo.

  Rwanda ukiiba pesa, hupewi muda wa kuzirudisha ili usamehewe. Pia Kamanda agame huwa hasemi ati ''nawafamu wezi wooote wa bandarini ila nawapa muda wajisafishe''.
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  If you want to walk on water, you must first step out of the boat!
   
 16. F

  Fikrasahihi Member

  #16
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siwezi kutoa hukumu ila sidhani kama maombi yenu yatazingatiwa kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka kutoka ktk chama chenu cha chadema hii inatokana na viongozi wenu kuwa wabinafsi katika madaraka pamoja na kushikilia ukabila wakati Baba wa Taifa alipiga vita sana ukabila sasa chadema muntaka kufanya nini, hewe mungu hata dua zao zisisikilizwe hata kidogo, na mwenyezi mungu mjaalie Mh.Jakaya afya njema na maisha marefu aweze kuongoza hii nchi.
   
 17. m

  maggid Verified User

  #17
  Oct 8, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Majibu yangu ya mada kutokana na kilichoandikwa na Gofrey Dilunga ( Raia Mwema)  Mtu mzima unaweza hata kujifunza kwa mtoto wa miaka sita. Unachotakiwa ni kuwa na utayari wa kujifunza. Kuna siku mtoto wangu wa miaka sita alinifundisha hili; “ Niliandaa uji wa ulezi wa asubuhi . Akawa wa kwanza kuamka kabla ya wenzake. Nikamwambia; “ Nenda mezani, chai tayari!”.
  Akaenda, baada ya sekunde chachea akaniita; “ Baba njoo!”
  Nikaenda, akaniangalia usoni na kuniambia; “ Baba hii sio chai, huu ni uji!”
  Nikakiri mapungufu. Na mapungufu yale kwangu ni ya kimalezi, wengi tunayo. Tukiwa kuruta JKT enzi nakumbukua na usomi wetu wa form six, pale kambini Itende JKT, baada ya mchakamchaka wa alfajiri na usafi tuliambiwa na Afande Paul; “ Kuruta nendeni mkanywe chai!”.
  Wote tuliokuwa pale Kambini Itende, wengine tumo nao humu JF ni mashahidi, kuwa pale Itende tulikunywa maji ya moto yaliyochemshwa pamoja na vumbi la kahawa na sukari. Haikuwa chai. Lakini ni nani kati yetu alithubutu kwambia afande Paul; “ Hii sio chai, ni kahawa, ingawa si kahawa hasa!”
  Tatizo hilo la kimalezi linatusumbua wengi wetu mpaka hii leo. Unaona kwa macho kuwa bwana mkubwa anakupa chungwa, halafu anakwambia pokea embe hili! Wewe unakubali!
  Mtoto wangu wa miaka sita anatupeleka kwenye kutafakari alichoandika ; Godfrey Dilunga; “ Nimeona waschotaka kukiona” ( Raia Mwema)
  Dilunga anaandika;

  “Nguvu ya utulivu na usikivu ya mkusanyiko wa watu zaidi ya 40,000 niliyoshuhudia Ifakara ndiyo iliyojitokeza Lupiro-Mahenge, Njombe, Songea na Iringa.”

  Anaendelea kuandika; “Kama leo mkusanyiko wa walalahoi zaidi ya 40,000 katika kila mkutano wanakua watulivu, ipo siku utulivu na usikivu ule utafanyiwa kazi na walalahoi hao hao. Siku hiyo itafika kama watawala watazidi kujenga wananchi wa mfano wa mama muuza ndizi.”
  Sasa hapa sijamwona aliyehoji na kudadisi uhakika wa anachokiandika Dilunga. Hivi ni kweli pale Ifakara Dilunga aliwaona watu 40, 000? Ifakara sikuwapo, lakini pale Mwembetogwa Iringa nilikuwapo. Watu waliofika pale hawakuzi 5000. Ukubwa wa uwanja wa Mwembetogwa na maeneo ya jirani hauwezi ukajaa watu zaidi ya 5000 na wakaweza kumsikia anayezunguza achilia mbali kumwona kwa sura.
  Ndio tatatizo letu, tunapenda kusikia tunavyotaka kusikia, na kuona tunavyotaka kuona. Shilingi ina pande mbili, tuwe na ujasiri wa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Ujasiri wa kuangalia tusivyotaka kuangalia, kusikiliza tusivyotaka kusikia. Sina cha kuhofia katika kuandika fikra zangu, maana ni fikra zangu. Fikra huru. Na najua kuwa mimi si malaika, nina mapungufu yangu. Ndio maana tukaitwa wanadamu. Najifunza kila siku, hata ninapokutana na mchoma mahindi Kitonga aliyeishia darasa la saba, naamini nina nitakachojifunza kutoka kwake. Na kwa mwanadamu, katika yote unayayotakiwa kuyakubali. Usisahau kuukubali ushamba. Nimezaliwa mjini na kukulia mjini, tena Ilala, Dar. Lakini siku zote natanguliza ‘ushamba ‘ wangu. Ndivyo nilivyo.
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe TAFAKARI ndiye unaonekana una matatizo -- au ya uelewa au ushabiki wa kijinga kwa JK. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakayeshindwa kutambua mapungufu makubwa katika utawala wa JK. Watu waliopevuka kama Mbwambo ndio wana uthubutu wa kuweka hayo wazi. Kumkosoa mtu haina maana kwamba una chuki naye kama binadamu. Yawezekana JK kama binadamu wa kawaida ni mtu safi, lakini kama kiongozi wa nchi ana maapungufu makubwa sana. Naamini Mbwambo atazidi kumchambua zaidi ili watanzania wasije wakafanya makosa ya kumrejesha madarakani mtu asiye na sifa ya kuendelea kuwa rais wetu. Unamwita Dr Slaa kama Padre Slaa. Mhariri wa Daily News katika ile tahariri yake ya kipumbavu pia alitumia neno Padre. Lakini Dr Slaa sio padre, na wewe unajua hilo. Ni dalili au ya udini au chuki tu za kijinga dhidi ya kiongozi huyu ambaye sasa anaonyesha kukubalika zaidi kuliko huyo JK wenu.
   
 19. F

  Fikrasahihi Member

  #19
  Oct 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yeye ni mwanadamu kama wengine anamapungufu sawa, lakini kwa nini aandikwe kwa mabaya kwani mazuri aliyoyafanya hamuyaoni?, kila mtu anamapungu hata weye kwenu vilevile unayao mapungufu huwezi kuwa mkamilifu mpaka unaingia kaburini hivyo watanzania wote tuungane, tushirikiane naye kuhakikisha mapungu tunayaondoa kwa kumpigia kura na kumweka madarakani, kisha ndio tuangalie maendeleo ya nchi yetu.
   
 20. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Gonga hapa chini usome article ya mbwambo inayomzuzua tafakari
   

  Attached Files:

Loading...