Y. Makamba na jedwali a mapusha wa cocaine! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Y. Makamba na jedwali a mapusha wa cocaine!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, May 20, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Wana JF, tusijisahaulishe!! Ikumbukwe kwamba Ufisadi kama ambavyo leo hii tunauita, ni hujuma iliyokomaa!!

  Duniani kote, mafisadi wakubwa (grand corrupts) ndio hao hao wanaojihusisha na biashara zingine haramu kama vile madawa ya kulevya zingine zinazofanana na hiyo!

  Kwa muda mrefu, TZ na TAKUKURU yake ilikuwa inaishia kwa wala rushwa uchwara (waganga njaa), kama vile mahakimu wa mahakama za mwanzo na manesi!! Angalau kwa sasa, tunawaona mafisadi wakubwa wakiumbuliwa na wengine kupelekwa mahakamani!!

  TAKUKURU na serikali, angalau wameonesha njia katika hili!! Vipi kuhusu taasisi ya kupambana na madawa ya kulevya? Inakuwaje hadi leo hii wanaishia kuwavizia wameza pipi pale Airport ambao wengi wao ni waganga njaa!!? Ina maana hawajui kwamba ukimkamata mmeza pipi mmoja wanazaliwa wengine mia moja?!Wako wapi wanaowatuma vijana hawa ambao kama ni ufisadi tungewaita ndio mafisadi papa!!

  Iko wapi ile list ya wakati ule tuliyoambiwa ilipelekwa kwa mheshimiwa Makamba!! Bado tu inafanyiwa uchunguzi? Au mheshimiwa nae kaingizwa katika jedwali la mapusha!!?

  Ufisadi nchi hii umeenea kila sekta, ingawaje tunavyoaminishwa ni kama uliokuwepo ni ule tu wa wanasiasa (political corruption)!! Aidha ikumbukwe kwamba, ufisadi kwenye sekta nyingine ndio unaohamia kwenye nyanja za siasa. Leo hii mkubwa (tuseme) wa jeshi la polisi anaeshirikiana na wauza unga wakubwa akipata utajiri wa kutisha, basi atajiingiza kwenye siasa ili akajitengezee kiota cha kuficha madhambi yake!

  Leo mfanyabiashara anaye-deal na biashara kubwa ya drugs akipata mafanikio ya kutisha basi lazima atajiingiza kwenye siasa ili akajifiche!! Kwani ni nani asiyeogopa kumchokonoa kigogo serikalini!!?

  Aidha, kwavile watendaji wa vyombo husika wanaonekana kulala usingizi,(si ajabu kwavile nao wamo katika jedwali la vigogo wa madawa ya kulevya!) basi (mimi binafsi , na wengine watakao) tunawaomba wakina Dk. Slaa watufichulie na vigogo hawa wa biashara haramu!!

  Nashawashika kuamini kwamba wakina Slaa waliwataja mafisadi kutokana na mapenzi waliyonayo kwa watanzania, na si kwa ajili ya kupata mtaji wa kisiasa pekee (aidhuru hata kama ndio main objective) !!

  Inawezekana kuwataja wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya usiwe mtaji mzuri wa kisiasa lakini itaonesha ni kwa jinsi gani wanafanya mambo yao kwa maslahi ya taifa!!
   
 2. N

  Nassoroc Member

  #2
  May 21, 2009
  Joined: Dec 20, 2008
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Drugs mkuu ni angle ambayo wanene kupitia sekta mbalimbali wanahusika!!
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mahakimu tusaidine kuutokomeza ufisadi unaitokomeza TZ.
   
Loading...