Xiaomi 13 Ultra specifications: Rumoured

hapoa nimekupata mkuu..naoana xiaomi mid range nyingi zinazo kuanzia 2.1
 
Xiaomi 13 Ultra: Official images
So beautiful
 
Kuhusu hii simu sijapenda muundo wa kamera hapo nyuma.
Nina swali pia. Sijajua tofauti sana kati ya xiaomi na redme.
Natumia redme 11. Ni nzuri ila kwangu ina changamoto mbili; haina kitaa cha notification kwa mbele. Pili kamera yake kwa upande wa kuchukulia video haiko smooth kabisa.
Naisifu kwa kukaa na chaji. Pia kioo chske ni imara sana
 
Hii simu hapo juu Inauzwa shs ngapi!?
 
Hicho kitovu ni cha nini
 
redmi ndio xiaomi wenyewe isipokuwa hiyo ni aina ya simu zao mfano xiaomi mi hizi ndio simu zao za flagship,poco,k,T,ndio zinafwata hizi mid-range za note yaani redmi note 10,11,12,alfu inafwata C na A mfano redmi 10C,redmi 9A
 
Xiaomi ni jina la kampuni inayotengeneza simu zenye brandname nne tofauti


1. Xiaomi
Xiaomi ni moja ya brand nne zinazotengeneza simu kutoka kampuni ya Xiaomi. Miaka ya nyuma brand hii ilikuwa inaitwa "Mi" ila kwa sasa inaitwa Xiaomi.
Brand ya Xiaomi inatengeneza flagship na flagship killers. Kwa mfano hii Xiaomi 13 Ultra moja ya simu kutoka brand hii. Pia inatengeneza Xiaomi MIX series. Licha ya kuwa brand ya Xiaomi inatengeneza flagship lakini pia inatengeneza midrange mfano Xiaomi Civi lakini hawatengenezi low end.
Hii ndio brand inayobeba jina la kampuni
Simu kutoka brand hii ya Xiaomi zinatumia software ya MIUI
Huu ni mwonekano wa MIUI kwenye Xiaomi 12S Ultra

2. Redmi
Redmi ime-base kwenye kutengeneza low end na midrange phones. Kwa mfano Redmi series ni low end za kampuni hiyo na huwa imegawanyika katika vanilla Redmi series, A-series na C-series. Mfano wa wa vanilla Redmi series ni Redmi 8, Redmi 9 na Redmi 10. A-series ni kama Redmi 8A, Redmi 9A na Redmi 10A, C-series ni kama Redmi 9C, Redmi 10C na Redmi 12C.
Hata hivyo Redmi ina simu za Note series ambazo ni midrange zilizobase kwenye kamera, display na SoC kwa bei rahisi mfano Redmi Note 11, Redmi Note 12, Redmi Note 10 Pro, etc.
Licha ya kuwa Redmi ime-base kwenye low end na midrange lakini pia Redmi hutengeneza flagship mfano Xiaomi Redmi K60 Pro ni flagship ya Redmi
Redmi ni brand ya Xiaomi inayoongoza Kwa mauzo kuliko brand zote nne
Simu kutoka brand hii ya Redmi zinatumia software ya MIUI kama.
Huu ni mwonekano wa MIUI kwenye Xiaomi Redmi Note 10 Pro

3. Poco
Poco haina tofauti kubwa na Redmi Kwa sababu ime-base sana kwenye low-end na midrange lakini simu za Poco ni popular sana nchini India
Poco hutengeneza low end kama Xiaomi Poco C40, pia hutengeneza midrange kama Xiaomi Poco X5 Pro na hutengeneza flagship kama Xiaomi Poco F4 GT
Simu kutoka brand hii ya Poco zinatumia software ya "MIUI for Poco". Tofauti ya MIUI for Poco na MIUI ya kawaida ni kwamba hii ya Poco, icons za apps zake zipo katika shape ya duara wakati kwenye MIUI ya kawaida icons zina shape ya square yenye rounded corners.
Ukiondoa hiyo tofauti kila kitu kinafanana na functionality yake ni same.
Huu ni mwonekano wa "MIUI for Poco" kwenye Xiaomi Poco M5

4. Black Shark
Hii ni brand inayotengeneza simu ambazo ni special for gaming
Kwa hiyo simu hizi zina chipset zenye nguvu kwa ajili ya gaming
Simu za Black Shark zinatumia software ya JoyUI ambayo imekuwa extracted from MIUI na kuwa modified ili iendane na gaming, Kwa hiyo ina gaming themes nyingi, gaming wallpapers na features nyingi za gaming.
Huu ni mwonekano wa JoyUI kwenye Xiaomi Black Shark 5 Pro
 
Loh! Thanks kwa somo makini
 
Sema disigner wa hii pc kaidisgne inaoneka ya kike. Hizi kwa % nyingi utawaona nazo wadada na wamama.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…