Xavi Hernandes astaafu

Xavi Hernandes astaafu

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
Kiungo wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Xavi Hernandez ametangaza kustaafu soka la kimataifa.
attachment.php

​

Hernandez mwenye umri wa miaka 34 alichezea timu yake ya Hispania na kutwaa ushindi na pia makombe mawili Ulaya akiwakilisha nchi yake.


Xavi amewaambia waandishi wa habari Barcelona jumanne hii kuwa ana furaha kutimiza kipindi chote cha kucheza soka hadi anapofikia kustaafu na kwamba kwa kipindi chote hicho amekuwa na wakati mzuri.


Akiwa na umri wa miaka 20 alianza kung'ara baada ya kuipatia ushindi timu yake katika mechi ya 15 Novemba 2000 ambapo Uholanzi ililazwa bao1-0 dhidi ya Spain.

Katika umri huo pia Xavi alikaririwa na vyombo vya habari akisema mie si mwenye miaka 20 tena lakini bado nina hamasa ya kitoto.

Hata hivyo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2008 katika ligi ya Ulaya wakati huo Hispania ikiwa inasubiri kutwa kikombe cha kimataifa baada ya miaka 44 tangu kung'ara kidunia.

Hispania ilianza kombe la dunia 2014 nchini Brazil kama moja ya timu maarufu na tarajiwa lakini wakatolewa nje katika hatua ya makundi baada ya kuchabangwa 5-1 na Netherlands na kisha 2-0 dhidi ya Chile.

Xavi mwenyewe pamoja na kutangaza kustaafu sasa amesema kuwa ilikuwa hatua hiyo aichukue 2012 baada tu ya ligi ya Ulaya lakini kocha wake Vicente Del Bosque alimsihi asichukue uamuzi wa kustaafu hadi baada ya Kombe la Dunia jambo ambalo la kuvunja moyo kwangu na kwa wengine pia.

"Nachukua fursa hii kumshukuru kila mmoja katika timu kwa jinsi walivyonichukulia na kuniheshimu".

Chanzo: BBC
 

Attachments

  • Xavi-Hernandez.jpg
    Xavi-Hernandez.jpg
    34.4 KB · Views: 201
A true living legend...

Mshindi wa Kombe la Dunia, Kombe la Ulaya na Kombe la Mabara...
 
Back
Top Bottom