X-Mas ilivyoniendea kombo!!!

HorsePower

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2008
Posts
3,612
Reaction score
2,569
Hbr wana MMU?

Ktk kipindi hiki cha mwisho wa mwaka pamoja na shamra shamra za x-mas na mwaka mpya, nilikuwa nimejipanga kupata muda wa kumshukuru Mungu kutulinda mwaka huu wote na kutuepusha na mabalaa na kisha kupata wasaa wa kuzunguka na marafiki zangu kadhaa sehemu mbali mbali za kuvutia na kuenjoy maisha!

Lakini kumbe mipango, si matumizi! Tar 23 nilipata taarifa kuwa mama yetu mdogo alikuwa akitoka mkoani kuja Dar akiwa na msichana wa kazi kuja kushehereka nasi na sikukuu za mwisho wa mwaka. Treni lilipofika pande za Dom ikasimama kwa ajili ya abiria kushuka na wengine kupata mahitaji mawili matatu kabla ya kuendelea na safari. Ma mdogo naye alishuka kwa ajili ya kununua vitu viwili vitatu, lakini bahati mbaya alianguka ghala. Aliwahishwa hosp kuu dom na kupelekwa ICU lakini baadaye alipoteza maisha. Manesi walifanya jitihida kuwasiliana nasi kupitia simu yake kupitia namba zilizohifadhiwa huko na kufanikiwa kutupata.

Tulifanikiwa kumsafirisha kuja Dar na tulizika tar 26. Tunashukuru kwa umati wa watu waliojitokeza kutufariji. Hii ilituthibitishia kuwa alikuwa mtu wa watu.
Mwenzenu niko chini bado naendelea kuomboleza kwa tukio hili zito lililotukuta. Pia nafikiria kumbukumbu aliyojijenga juu ya msichana huyu wa kazi aliyeondokewa na mwenyeji wake akiwa safarini asijue wapi pa kwenda na nini cha kufanya. Mungu amfariji pia kwa magumu yaliyomkuta. Nitumie muda huu pia kuwapa pole wana JF wote walipoteza wapendwa wao mwaka huu wa 2012. Mungu aendelee wakuwafariji na kuwatia nguvu.

Nilichojifunza:
Maisha ya mwanadamu ni kama maua, asubuhi yanachanua na jioni yananyauka. Hivyo basi, ni vyema kwa kila mtu kwa imani yake kuishi ktk maisha ambayo yanampendeza Mungu wake. Tujitahidi kutenda yaliyo mema, na pia kuwa tayari kusamehe na kusahau mabaya tuliyotendewa. Hii uitasaidia tunapokutana na tukio kama hili tuweze kuagwa vyema na kuacha kumbukumbu njema kama wapendwa wetu walivyoagwa. Tunapousogelea mwaka 2013, tuusogelee tukiwa na mitazamo wa kutokuwatenda watu mabaya. Tujitahidi kuishi kwa amani huku tukikwepa vurugu za kidini, kuacha ufisadi, rushwa na mabaya mengine yote yanayofanana na hayo. Pia tuwe wavumilivu kwa wanaotutenda mabaya na kuwareport kwa vyombo husika badala ya kuchukua sheria mkononi.

Nawaombea dua Mungu awalinde na kuwavusha na mwaka huu wa 2012 na hatimaye tuingie mwaka 2013 tukiwa na afya njema. Nawatakia baraka, mafanikio na ushindi ktk kila mfanyalo.

Wenu ktk maombolezo,

HorsePower
Dec 2012.
 
Very well spoken mkuu. Yote ulionena yana mashiko.

R.i.p mama mdogo, Mungu amsamehe mabaya yake yote aliyotenda enzi ya uhai wake
 
Mkuu HorsePower pole sana, Mungu azidi kukutia nguvu. Asante sana kwa maneno yako ya busara kwetu, asante sana.
 
Pole sana sana HorsePower. Kweli ni tukio linalosikitisha sana na kutia majonzi. Mungu awape faraja mioyoni mwenu, na muachieni Mungu na tujifunze kushukuru kwa kila jambo kwani ndivyo maandiko yanavyosema.

Hata hivyo, mimi naona tujifunze sana kuwa na hofu ya Mungu wakati wote maana hatujui ni lini mwisho wa safari yetu. Na tusifanye hivyo kwa lengo la kuagwa vema kama ulivyosema kwani kuagwa vema hakutatusaidia iwapo Mungu hatutambui, ila tufanye hivyo kwa lengo la kumpendeza Mungu ili atukumbuke katika ufalme wake, nadhani hilo ndilo la msingi
 
HorsePower pole sana na yaliyokukuta. Pole kwa kumpoteza mpendwa wenu.
Sasa huyo housegirl ndio kaishia wapi?
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu,ahsante kwa ujumbe mzuri wa kututia moyo!

Mungu akupe nguvu zaidi na uvumilivu ktk kipindi hiki cha majonzi!

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi,amen!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Maskini, ndio maana ulikuwa huonekani MMU. Pole sana kwa kuondokewa na mamdogo.

Ni kweli maisha yetu ni mafupi sana, na tungejua tusingekuwa na majivuno ya kuzidi.
 
Du usilolijua ni kama usiku wa giza,tungekua tunajua mwisho wa maisha yetu sijui ingekua vipi,,sometimes hua nawazaga haya tunayoyatafuta magari,nyumba,nguo si lolote yanapita vuupu kama upepo bora sanyingine tujiandalie hazina ya badae kulingana na imani za kila mmoja wetu,,ila shetani hakawii
 
Pole sana kwa yaliyokukuta na amani ya Mungu ipitayo fahamu zote na iujaze moyo wako, asante kwa kutukumbusha kutenda mema.
 
Pole sana kwa kumpoteza mama mdogo..! Duniani tu wapitaji.. R.I.P Mama mdogo!!
 

Aine, Asante kwa ujumbe mzuri
 
Last edited by a moderator:
Duuh pole mwaya ila huyo housegal kama asingekua mvumilivu aisee cjui nini kingetokea , usiombe kuondokewa na mtu mikononi mwako
 
HP mungu awape faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
 
Pole sana HorsePower .. Mungu akujalie nawe usahau machungu haya. Asante pia kwa ujumbe mzuri.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mkuu HorsePower, namuomba Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya mama yetu mdogo na pia kuwapa nguvu na faraja katika kipindi hiki kigugu kwenu~AMEN.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…