Mkuu nimesoma lakini nimepata ukakasi sana,
Henry Kissinger ni mkorofi lakini hawezi kusema haya maneno hadharani hata siku moja: Haingii akilini mtu ambaye ndiye mjenzi wa Sera ya
DETENTE na amefanya diplomasia kipindi cha Vita Baridi ambacho kiliwahi kuwa hatari duniani aropoke ujinga wa namna hii tena kwenye mahojiano ya hadharani. Ndiyo yale yale ya kusema Donald Trump kasema Afrika inabidi itawaliwe tena. Kitu kikubwa Henry Kissinger hawezi kuongea ujinga wa namna hii ambayo ni mawazo ya mwenda wazimu.
Mwezi January
Secretary Henry Kissinger na
George Schultz waliitwa kwenye Bunge la Marekani kuzungumzia hatari zinazoikabili Marekani kwa kipindi hiki. Walitaja Islamic Fundamentalism na Lethal Weapons Proliferation, ambapo Schultz alisema "Our enemies manufacture weapons which are Cheap and tiny but very lethal" huku Henry Kissinger akiitaja Urusi kwa kusema "Russia is a very weak country with massive military establishment". Leo hii mtu kama huyu hiingii akilini asema kwamba Urusi watapigwa kirahisi na NATO na ISRAEL.
Mwaka jana Henry Kissinger alizungumzia tena sera yake ya
Divide et Empera kwamba Marekani na Urusi zinahitajiana kwa kipindi hiki kigumu. Kama Marekani anataka kuua ushawishi wa Uchina basi hana budi kuungana na Urusi kwasababu wao pekee ndiyo wanaweza kuzuia kabisa nguvu ya kijeshi ya Uchina inayokua kwa haraka. Huku wataalamu kama Prof.
Graham T Allison alipohojiwa kuhusu uhusiano baina ya Taifa la Urusi na Marekani hakutofautiana sana na Henry Kissinger alisema kwamba "
America and Russia are like Siamese Twins" kwamba wana mlengo moja na maono sawa hivyo wanavyopigana hapa wanajichelewesha huku adui yao Uchina anakua kwa kasi sana.
Kubwa zaidi kuthibitisha kwamba hili bandiko ni la Uongo, kwa tuliosoma Sayansi ya Siasa tunajua kwamba kuchambua kwamba Dr. Henry Kissinger anatoka kwenye School of Thought ambayo inaitwa
A REALIST SCHOOL OF THOUGHT. Ambao watu kama Dr. Henry Kissinger na
Prof. John Mearshimer wanaamini kwamba The World Order is built on a foundation of The Balance of Power.
FULL STOP. Haijalishi nani mbaya na nani mzuri cha msingi ni kwamba kutakuwepo na amani ya dunia pale tu ambapo mzani wa dunia una uwiano linganifu. Katika hali hiyo basi, hawa Realists wanajua ukweli moja mchungu kwamba "
Siyo rahisi taifa moja kuwa kiranja wa dunia bila kuleta matatizo makubwa ka vita zisizoisha"
Kuna siku moja alikuwepo Canada kwenye
The Munk Debates, yeye pamoja na
Fareed Zakaria,
Alisema kwamba Kama Vita inatokea basi Uchina hawezi kuzuiwa kirahisi hasahasa Barani Asia kwasababu katika nchi zote zinazomzunguka China hakuna hata moja inaweza kupigana naye. Sasa sijui huko kuwaua Wachina na kuwageuza majivu sijui kunatokea wapi....Teh teh teh teh teh teh.
Ili kupigana na Uchina kwa ushindi inabidi Marekani apigane The Second Pacific War na Uchina kama alivyopigana na Japan kwenye vita ya pili ya dunia, kitu ambacho kwa saa hizi sidhani kama ni kirahisi kihivyo na wala siyo leo wala kesho.
Steve Bannon alinukuliwa akisema in "Five to Ten years we will be going to war with China" Sababu kubwa ni kwamba kipindi hiki nguvu ya jeshi ya Marekani kule ukanda wa Pasifiki imepungua sana na Dr. Henry Kissinger na American Security Establishment wanajua kabisa IT WILL BE SUICIDAL TO GO TO WAR WITH RUSSIA AND CHINA in the Pacific. Kipindi cha Raisi Ronald Raegan ukanda wa Pasifiki ulikuwa na Manowari za vita kama 600 za kisasa kabisa ambazo zilikuwa zinatuma ujumbe kwa Wasovieti na Wachina kwamba mkifanya Ujinga huu ukanda tunawamaliza.
Lakini kipindi hiki Marekani ina meli vita kama 300 tu kwenye ule ukanda wa Pasifiki (Japo ni za Kisasa sana) huku Uchina ikijijenga sana na kuongeza idadi za manowari na kutanua visiwa (Artificial Islands) huku wataalamu wa The Washington Post wakisema kwamba
China Will have more Warships than the US in 2020: Soma hapa ujionee mwenyewe kilichosemwa:
China will have more warships than the U.S. by 2020, says report Huu ni ukweli mchungu ambao hata Henry Kissinger anaujua. Sasa kuleta huu ujinga kwamba Henry Kissinger anasema kwamba watamzika Uchina wakati Donald Trump na wenzake wameanza kujenge upya jeshi la Marekani kule Pacific..Teh teh teh teh teh mimi nacheka sana na kuziba mdomo tu. Kibaya zaidi ukute kuna baadhi ya watu wameamini hichi kilichoandikwa hapa.
NB: Mashariki ya kati kuna vurugu mpaka sasa kwasababu mpaka sasa kati ya Mataifa yenye nguvu ule ukanda:
Israel,
Misri,
Uturuki,
Iran na
Saudi Arabia hakuna hata moja ambaye amafanikiwa kumshinda mwenzake kikamilifu hadi kumpata mbabe kati yao. Iwe ni Iran au Israel wote wanategemea mataifa ya nje kama Marekani na Urusi na hawawezi kuanza Ujinga bila kuruhusiwa na Bwana zao. Ndiyo maana nasema kwamba kama Israel angekuwa na huo uwezo wa kutawala nusu ya Mashariki ya kati basi angeshafanya hivyo muda sana na hata huyo Assad angekuwa ameshakufa muda mrefu, na majimbo angenyang'anya kama alivyofanya kwenye
Six Days War au
Yom Kippur War lakini bahati mbaya sana kama akilianzisha anaweza kukutwa na majanga hayo ambayo, GOD KNOWS ni mabaya sana na itakuwa MASSACRE pale.
CC:
Consigliere ,
izzo ,
chige ,
TUJITEGEMEE ,
MASAMILA ,
Maalim Shewedy