Wosia wangu kwa vijana wa kiume humu JF, huenda nisitoe tena wosia huu

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
3,979
5,295
Vijana! Nguvu kazi ya taifa letu, watoto wetu, wakwe zetu, madaktari wetu, wanasheria wetu.

Kijana, nakuambia leo hii Jumapili, usipojipenda hakuna wa kukupenda niamini mimi. Huwa nalia machozi kuona vijana wanahangaika kila siku kuwafurahisha na kuwaridhisha wasichana. Unashindia mihogo, yeye anakula burger. Unavaa hovyo ili yeye apendeze, unakonda ili anenepe. Idiot!

Siku hizi vilio vya wanaume ni vingi mno, hususani vijana. Hela zako, pesa zako, ulitafuta mwenyewe, ila bado mtu anakula hela zako huku wewe unakonda, na mbaya zaidi anakuliza, anakunyanyasa, anakufedhehesha, haoni thamani yako na bado anatumbua hela zako. Ni upuuzi. Halafu unalia lia hujui cha kufanya?

Kijana wa kiume popote ulipo mkoa wowote, kona yoyote ya Tanzania hii na hata dunia. Ni marufuku kuanzia leo kulia lia kwa sababu ya mwanamke. Umeharibikiwa maisha yako kwa sababu ya kumfurahisha mtu( mwanamke), aidha umefeli chuoni, umefukuzwa kazi n.k, pole fuatilia ili upone.

Unavaa 'crazy'(majina ya vijana) ili umvutie mwanamke, una fake kula migahawa ya gharama ili umvutie mwanamke na uonekana mjanja, unavaa mlegezo ili umvutie mwanamke, huli baadhi ya vyakula ili umvutie mwanamke, huendi baadhi ya sehemu muhimu ili umvutie mwanamke, huongozani na baadhi ya watu 'potential' kwako ili umvutie mwanamke, endelea kusoma

Umegombana na marafiki waliokutakia mema, waliokuambia ukweli pale ulipokosea, ili umfurahishe 'demu' wako. Hiyo ni laana!

Kisa utaonekana mshamba au wa hadhi fulani. Unawakwepa baadhi ya marafiki potential na wanaokuwazia mema ili umfurahishe mwanamke.

Umeshindwa kulipa fadhila kwa kuwasaidia marafiki waliokushika mkono ukiwa huna kitu, ukiwa unatoka kamasi kwa kupigwa na maisha, ukiwa sio wewe uliye leo hii, ili kumfurahisha mwanamke. Amekukataza kuwasaidia ,eti si watu wazuri kwako.

Kwa mwanachuo, unashindwa kuchangamana japo kidogo tu na wanaume wenzio fulani kisa unawaona washamba, unaogopa unayemuita 'demu' wako atakushusha hadhi kwa kupiga hata stori tu na wanaume wenzako, eti kisa hawajui kuvaa kama wewe, hawana macho matatu.

Hao hao wenzako unaowadharau ndio watakaokushika mkono siku maisha yamekuchapa na kamasi zinakutoka mfululizo.

Heshimu wenzio, mwanamke asikupelekeshe KAMWE ukamdharau mwanaume mwenzio. Ni laana!

Jambo la kusikitisha ni kuwa tayari mpaka dakika hii udhaifu wenu umeshajulikana nao, kwa lugha nyepesi ni kwamba wengi wenu mpo uchi hata mkivaa nguo, yaani uchiiii ile completely. Wanajua wakilia kinafiki au kukohoa kidogo hamna amani.

Wanajua wakipiga simu kukuomba hela kubwa huna jeuri ya kupindua na upo tayari kuweka kiwanja cha urithi bondi, wanajua wakiwajibu shit hamuwezi kuwaacha, zaidi nyie ndio mtaomba radhi ili yaishe.

kuanzia leo;

Ni marufuku kijana wa kiume kulia lia kisa msichana, iwe kulia moyoni au mdomoni, ni marufuku.

Kuanzia leo anza kujipenda na badilisha lifestyle yako, kula vizuri, vaa vizuri, fanya kazi, soma kwa bidii, na ukipata hela jipe raha wewe KWANZA 80%, 19.9% kwa wazazi na ndugu, 0.1% kwa msichana. Hii itakujenga na kukujulisha usichojua, na utakuja kunishukuru kama nitakuwa hai.

Nenda restaurant agiza chakula, kula kwa raha zako, tembelea wahitaji waguse kwa hata kidogo ulichonacho.

Kaulimbiu;
1. Jipende 2. Jipende 2.5. Jipende 3. Mpende.

Kubali kuonekana mbinafsi, kubali kuitwa mchoyo, kubali kuambiwa unaringa, kubali kuitwa vyovyote, utapona wewe sio wa kwanza kuitwa hivyo.

#MkomboeKijanaWaKiume
 
Back
Top Bottom