WOSIA WA BABA...

WOSIA WA BABA...

Joshua justine

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
788
Reaction score
1,015
Ilikuwa ni familia yenye amani , upendo na furaha. Lakini watoto wote hawakuwa sawa, baba aliwajua watoto wake vyema . Kabla hajafariki baba wa familia aliwaasa wana familia yake ya kuwa mtoto wake fulani hafai na asiachiwe kushikilia maslahi ya familia, ila kwa dharau ama kwa ujinga baada ya kufariki mzee yule wale watoto hawakukumbuka mausia yale , kijana yule aliachwa akaitawala familia ile,mambo ya kutapanya mali za familia ,ule i na anasa za kila namna ndio vilitawala.
Watoto wale ajabu yao , wakampenda sana kijana yule naye akatumia mwanya huo kuiharibu hali yote ya utulivu wa familia ile . Mbaya zaidi ni pale yule kijana alipopata hawara yake , akampa kazi ya kusimamia familia ile pindi yeye mwenyewe anapokuwa hayupo , jambo hili liliwakera mno wanafamilia wengine hatimaye famila imeparanganyika na leo hawaelewi hatima yao.
WOSIA WA BABA YAO NI LAZIMA UWATAFUNE, NA MIMI NASEMA WACHA UWATAFUNE.
 
Back
Top Bottom