Wolper anusurika Kupigwa Risasi Kituo cha Mafuta

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487


Msanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati alinusurika kupigwa risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa kwa sababu za kipolisi) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa mgogoro mzito eneo hilo,

Tukio hilo lilijiri muda wa saa tano usiku Juni 12, mwaka huu ambapo mlinzi wa "sheli" hiyo almanusura amfyatulie Wolper risasi baada ya kutokea sintofahamu kati ya Wolper na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho.

“Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale 'sheli' akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab Abdulkan).

“Akaongeza mafuta na kuondoka zake, dakika kadhaa baadaye, tulishangaa kumuona Wolper akirudi tena na kwenda mpaka kwa yule dada aliyemuuzia mafuta lakini safari hii alionekana kuja kwa shari.

“Akashuka kwenye gari na kuanza kumuwakia yule dada kwa madai kwamba amemuibia mafuta na kusababisha gari lake limzimikie njiani wakati alitoa shilingi elfu ishirini,” alieleza shuhuda wa mkasa huo.

Kwa mujibu wa shuhuda huyo, mgogoro mzito uliibuka eneo hilo baada ya msichana huyo kumjia juu msanii huyo ambaye hakukubali, ndipo Wolper akaamua kumvaa mdada huyo na kuanza kumshushia kichapo, tukio lililokusanya umati wa watu.

Baada ya purukushani hiyo ya muda mrefu ilibidi mlinzi wa kituo hicho cha mafuta, aingilie ugomvi huo. Hata hivyo, mlinzi huyo alionekana kumtetea zaidi mfanyakazi mwenzake na kumkandamiza Wolper, jambo lililozidi kumpa hasira msanii huyo.

“Alipoona wanasaidiana, Wolper aliwachenjia wote wawili, jambo lililosababisha mlinzi huyo aondoke eneo hilo lakini aliporejea, alikuwa na bunduki yake ya lindo mkononi, akaikoki na kutaka kumpiga risasi Wolper,” alieleza shuhuda huyo na kuongeza

Kuona hivyo Wolper alikimbilia ndani ya gari lake na kutoka nduki, akiacha watu wengi wakiwa wamekusanyika kituoni hapo.

Wolper alipotafuta kuzungumzi kadhia hii alikiri kutokea kwa tukio hilo.

“Dah, ni kweli nilikutana na matatizo hayo usiku, ambapo nilikuwa naenda Tegeta baada ya kufika njiapanda fulani pale, gari lilipungua mafuta nikaingia kituoni na kuongeza ya elfu 20, wakati naongeza nilihisi kabisa yule dada ananiibia lakini sikumjali, nikalipa na kuondoka.

Nilipofika mbele kidogo tu gari lilizima,” alisema Wolper na kuongeza: “Ilibidi nifanye utaratibu wa kupata mafuta mengine kisha nikageuza na kurudi mpaka pale sheli kwa lengo la kudai haki yangu ndiyo kukatokea timbwili hilo kwani mlinzi wa pale alikuwa anamsaidia yule dada aliyeniibia.”

“Wakati nikiwa najihami maana yule mlinzi alikuwa akinikaba, nilimpiga kibao, akakimbilia bunduki yake na kuanza kuikoki akitaka kunipiga risasi.

“Baada ya kuona amefikia hatua hiyo niliingia haraka kwenye gari langu na kuondoka zangu kwani nilihisi walikuwa na njama moja ya kuniibia mafuta na walipoona nimerudi kulalamika ndiyo wakaamua kunifanyia vurugu, kweli sikufurahishwa na tabia yao kwanza ni wezi wakubwa wa mafuta hao,” alisema Wolper.

Source: Bongo Movie
 
Pole yake ndio maana mimi huwa naweka kwenye kidumu kisha ndio naenda kuweka kwenye gari, siwaamini hao wafanyakazi hata kidogo ni wezi balaa.
Kuna kipindi hii ya kuweka kwenye idumu ilizuiliwa.

Vipi siku hizi wanaruhusu tena??
 
Wabongo bwana .. Sasa wanafhani Wolper atarudi tena hapo? Kitu kidogo sana ila kinaweza kuikost biashara.. Then wakiajiriwa wahindi basi malalamisha tele
Wanaofanya hivyo ni wafanyakazi mkuu , ambao kwao cha muhimu ni mshahara wao si biashara inaingiza nini.

Wafanyakazi wa ibongo wengi si waaminifu, biashara nyingi sana wanaziharibu wao, hata kama management iko vizuri.
 
Basi mwenzio nilitarajia chini kukuta sentensi 'katika muvi hiyo inayotarajiwa kutoka wiki ijayo Wolper amshirikisha Steve Nyerere na itasambazwa na Steps entertainment '..........

Maisha ya wasanii wa bongo ni usanii tu hata kwa mambo ya kawaida yaani
 
Basi mwenzio nilitarajia chini kukuta sentensi 'katika muvi hiyo inayotarajiwa kutoka wiki ijayo Wolper amshirikisha Steve Nyerere na itasambazwa na Steps entertainment '..........

Maisha ya wasanii wa bongo ni usanii tu hata kwa mambo ya kawaida yaani
Hapana mkuu

Hili ni tukio la kweli kabisa
 
Back
Top Bottom