kunze
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 398
- 470
Toka kwa mama yangu Heriety Chumira, Habarini za asubuhi wapendwa wangu? Huyu kaka anaitwa Zuberi Auli Zuberi, binti yangu jana jioni saa 12 alirequest bolt kutoka Yombo kwenda Kinyerezi, unaporequest inatokea picha na namba ya dereva kwa bahati nzuri binti yangu alimfananisha dereva na kaka wa rafiki yake hivyo akasrceen shoti hiyo picha na kumtumia rafiki yakr kumuuliza kama huyo ni kaka yake, kumbe ni Mungu tu alitaka picha ya kaka awe nayo, walivyofika mitaa sitakishari akawa anampitisha njia za vichochoroni hali imliyomtia wasiwasi binti yangu na kumuuliza kulikoni wanapita njia za ndani ndani wakati barabarani hakuna foleni dereva akadai anaogopa traffic kwakuwa hana leseni, kufika mbele kidogo akazima gari na kusema anahisi mafuta yameisha binti yangu akaanza kupata wasiwasi na kumuuliza dereva kulikoni lakini akamwambia binti yangu ashuke asukume hili ikiwaka wafike barabarani kuna petrol station baada ya binti yangu kushuka dereva aliwasha gari akaondoka ndani kukiwa na pochi yenye oesa, simu mbili vitambulisho vya benki ya CRDB, NMB, Kitambulisho cha Taifa chake na cha binti yake na documents mbalimbali. Amefungua kesi STK/RB/9567/3921 kituo cha polisi sitaki shari Heriety Chumira] @jenniferkyaka @wema_emily @halimayahya