mchekanapori
Member
- Aug 3, 2012
- 50
- 51
Habari wana jamvi, naomba ushauri wenu. Ndugu yangu alikuwa anakwenda benki ku deposit mamilioni kadhaa kutokana na biashara zake, alitumia usafiri wa pikipiki yake mwenyewe akiendesha, kufika eneo la benki akakutana na gari ya polisi wakamkamata na kumpeleka polisi, wakamvua kila kitu na wakachukue zile pesa na hata hawakuziandika pale kuwa amekuja na pesa kiasi gani, wakambambikia kesi ya kuandamana, kapigwa faini tena laki 3, alipouliza pesa zangu zipo wapi? Polisi wamemkatalia kuwa hajakuja na pesa kituoni, jamani hii nchi yetu inaelekea wapi, naomba msaada wenu tafadhalini.