Wizi wa Salio mtandao wa Voda

Wizi wa Salio mtandao wa Voda

Jt jr

Senior Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
181
Reaction score
57
Habarini ndugu zangu,

Jamani huu mtandao wa voda kulikoni?Juzi niliweka vocha ya 500 wakalamba 100, data zote ziko off.

Sikuwapigia sababu nilikuwa bize. Sasa jana kuna mtu kanipa nimwekee vocha ya jero then nimuunganishe, ile kumuunga naambiwa huna salio la kutosha, kucheki wamekata 100.

The same today jamaa kaweka jero kuunga eti salio halitoshi.

Sasa naomba watuambie hizi mia mia za watanzania masikini wanazipeleka wapi na kwanini?

Mbaya zaidi siku hizi hakuna kifurushi cha chini ya 500 cha dakika. Kwa hiyo wakikata hiyo mia unalazimika kununua vocha ya jero ili hata ile 400 isiibiwe.

Ndugu zangu huu wizi nimechoka, nahamia IST!

Nawasilisha
.
 
Wateja milioni 12 x sh100 = Tsh bilion 1.2

Tsh bil. 1.2 x siku 360 =
.....
@ vocha/day

kweli ni zaidi ya escrow
 
Vumilia mkuu, Mimi juzi nimeweka 25,000/= nijiunge kifurushi cha data cha mwezi nikaambiwa salio halitoshi, kucheki salio limebaki 24,900/= so ikanibidi niongeze jero ili kujiunga. Ikabaki 400/= nayo baada ya siku tatu nikakuta wamelamba yote japokuwa sikuitumia kwa namna yoyote hata kupiga simu ama kutuma text.

Nashindwa kuelewa hizi mia mia wanakata za nini! Huu ni ufisadi mkubwa sana zaidi hata ya escrow.
 
Mmmh mie ist siku nyingi huyo Jay millionea wabakinae wao mie akuu sitaki kuwa millionare
 
pole ndugu kama data ilikua off cheki labda umejiunga na simu tv maana nao kuna wakati hua wanakaa kimya ila day wakiamua vuna ni balaa. Kama hujajiunga basi ni wezi tuu
 
Vumilia mkuu, Mimi juzi nimeweka 25,000/= nijiunge kifurushi cha data cha mwezi nikaambiwa salio halitoshi, kucheki salio limebaki 24,900/= so ikanibidi niongeze jero ili kujiunga. Ikabaki 400/= nayo baada ya siku tatu nikakuta wamelamba yote japokuwa sikuitumia kwa namna yoyote hata kupiga simu ama kutuma text.

Nashindwa kuelewa hizi mia mia wanakata za nini! Huu ni ufisadi mkubwa sana zaidi hata ya escrow.

Hahahaha dah pole kamanda mm nshai kuta sana, mpaka nikasema siku nkikutana na mkurugenzi wa voda lazima niliye naye maana washatufanya sisi mambwiga
 
pole ndugu kama data ilikua off cheki labda umejiunga na simu tv maana nao kuna wakati hua wanakaa kimya ila day wakiamua vuna ni balaa. Kama hujajiunga basi ni wezi tuu

jamaa na anatumia nokia ya tochi harafu hana habari hizo. cha ajabu cm za watu watatu zimekatwa the same amount. ntabaki nawatrust kwenye mpesa tu
 
pole ndugu kama data ilikua off cheki labda umejiunga na simu tv maana nao kuna wakati hua wanakaa kimya ila day wakiamua vuna ni balaa. Kama hujajiunga basi ni wezi tuu
Hata Ukiwa na kitochi wanakula hela, usipojiunga jiunga
 
ever heard of privacy, most people don't like to reveal their wealth to the public, its a private matter in most countries, look at the Italian scandal of today regarding publications online! I bet even if the SFO clear this man you'll still find another pivothole to condemn him cause its a sin to be comfortable in Tanzania apparently

You made my day...Jay Millions umemchoka?...au hamia Zantel/Tigo
 
Duh! kumbe mode wa jf wanaedit post zetu! maana title ya hii thread imebalishwa km dakika tatu baada ya kupositiwa. kweli kazi wanayo maana post zote hizi km wanazisoma kweli wako serious na kazi.
 
Sio vodacom peke Yao hata tigo nao wanaibia wateja. Mimi huwa wananikata 150 kila siku na sijui sababu za wao kufanya hivyo. Kwa sababu sijajiunga na huduma zozote zile za tigo zenye makato
 
Sio vodacom peke Yao hata tigo nao wanaibia wateja. Mimi huwa wananikata 150 kila siku na sijui sababu za wao kufanya hivyo. Kwa sababu sijajiunga na huduma zozote zile za tigo zenye makato

TCRA sasa wanafanya nn kweli haya matatizo hamna hata ndugu yao aliyekumbana nayo? labda yeye wangemsikiliza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom