Wizi wa Mtandao (ATM) unaotokea katika banki ya NMB tawi la Benki House Dar es Salaam

displayname

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
1,950
1,039
Habari wanajamvi,

Nimeona niwashirikishe wadau naona tangu pesa iwe adimu awamu hii ya tano kama wengi wanavyo amini hivyo, (mimi si mwamini wa hayo) kumekuwepo kwa matukio ya wizo wa fedha hasa katika Benki ya NMB.

Pana jamaa zangu kadha wamepigwa pesa mwezi huu wa tano wote toka akaunti za NMB na wote ni watumishi wa Serikali na matukio yote yamepigwa katika Benki House Dar es Salaam, kupitia ATM mashine tena nyakati za usiku.

Niliopata taarifa zao waliibiwa;-
Mtu wa 1. 700,000
Mtu wa 2. 300,000
Mtu wa 3. 300,000
Mtu wa 4. 200,000
Mtu wa 5. 500,000
Hao ni baadhi ya jamaa zangu tu wakaribu niliopata sikia wakilalamika>

Mazigira ya kuibiwa yalikuwa hivi
Pesa zote zimetokea nyakati za usiku wakiwa majubmani mwao, ila wakapokea ujumbe mfupi (sms) kwamba kadi namba yako inasihia na.....imetoa pesa kiasi cha shilingi tajwa hapo...kwa kila mmoja wajua ule ujumbe unavyomalizikia kwamba kama hutambua muhamala huu piga simu namba....jamaa huyo Namba 2. 3000,000 pasipo kupoteza muda akapiga simu akawataarifu banki, nao wakamjibu aende kesho katika tawi lililo karibu nae.

Palipo kucha akafanya hivyo banki wakaiblock akaunti yake na wakaprint taarifa fupi ya akaunti ya jamaa, kweli ikaonekana kadi yake imetoa kiasi hicho cha pesa katika moja ya ATM iliyopo Banki House jijini Dar es Salaam.

Maswali ya kujiuliza hapo sasa?
· Kwa nini wote ni watumishi?
· Usalama wa fedha zetu NMB sasa ni wamashaka? tangu wazindua huduma za VISA/MASTERCARD? Japo wakati fulani pesa nyingi za akaunti za NMB ziliibiwa sana na watumisha wa VODACOM kwa huduma ya NMB MOBILE hadi kufikia wateja wa NMB kukataa huduma ya NMB mobile na kisha baaadae VODACOM wakapiga biti kali na kuwachukulia hatua watumishi waliobainika kuhusika na wizi huo.
· Kwa nini Benki House tu imehusika na matukio yote? tena usiku tu?

Baada ya kutoa taarifa benki, wao hadi leo akaunti hizo zimefungwa na kushusu kurudishwa fedha zao wanasema hadi watakapo anza kulipa kwa batch.

Bado na jiuliza je wizi huu unafanyikaje pasipo kufanywa na watumishi wenyewe wa benki ya NMB? Hivyo benki wanawajibu wakujichungiza, sina hakika kama nihujuma ila mashaka yangu ni wale waliozoeapiga pesa kidezo dezo sasa wameamua kujihusisha na uhalifu huo ili tu kuendele piga raound za Heineken kwenye viti virefuu.

Tahadhali!
Wenye akaunti benki zao NMB ni vyema mkafanya uhakiki wa salio lako mara kwa mara, ili kujua kama na wewe hao wasio waaminifu wamekutembele au lah! Au ukahamisha fedha zako katika benki yenye usalama wa hali ya juu.

Kama kuna wengine walioukmbwa na janga hili tushirikiane uzoefu na kupeana taarifa tuweze jua ukubwa watatizo hili!

UPDATES.....
Nimetoka bank NMB kwenda tazama salio langu nimekutana na mtu amepigwa milioni 7 ni pesa alizokopa benki, inaonekana benki walisha zitoa kwenda kwa akaunti husika ila hao wapiga dili wakazichota juu kwa juu kabla ya mwenye mkopo kuuchukua!!

Analia kama mtoto mdogo aisee....wezi muwe na huruma basi kiducho.



 
kunasiku nilikuwa na draw tsh 200000,ikatoka 260,000 then sms ikasema ndugu mteja account yako imetoa tsh 200,000 ,nikahesabu mara mbili mbili naona bado 260000. kuangalia risiti inasoma 200,000
nikaona ngoja nisepe nazo weekend ilikuwa poa sana hiyo.........
 
Duh hata mashibe hukosea... na wala hawajawahi kukusumbua hao jamaa?!
Una zari kweli aisee!
 
Cash Machine za bongo zote mbovu tu siku zingine naendaga kutoa hela nakuta wakati pale inafunguka ili itoe hela kuna hela zingine nyingi kwa ndani kama mtu una tamaaa unaweza kuzivuta na zile zingine....kwa kutumia kijiti tu....
Bro kamare si itakunyaka ukiichokonoa na ukajikuta matatani labda kama zile CCTV wameziweka kama bosheni tu
 
Hivi wabongo tuna shida gani? Kwanini mtu anapoelezea habari ya maana lazima atokee limbukeni mmoja aweke hadithi yake ya kujidai ili aonekane zinga la janja kumbe ni limbukeni? Sasa ulichoandika kina uhusiano gani na thread?
 
Hivi wabongo tuna shida gani? Kwanini mtu anapoelezea habari ya maana lazima atokee limbukeni mmoja aweke hadithi yake ya kujidai ili aonekane zinga la janja kumbe ni limbukeni? Sasa ulichoandika kina uhusiano gani na thread?
kwani kuna tatizo dada? tuna share uzoefu
ila sawa nimekuelewa muungwana.
 
Hivi wabongo tuna shida gani? Kwanini mtu anapoelezea habari ya maana lazima atokee limbukeni mmoja aweke hadithi yake ya kujidai ili aonekane zinga la janja kumbe ni limbukeni? Sasa ulichoandika kina uhusiano gani na thread?
Mkuu mimi naona usiangalie tu kilichoandikwa pale mwishoni mwa post ya mchangiaji.

Kwa kuzingatia kwamba mada inahusu upotevu wa fedha za wateja kupitia ATM mchangiaji huyo nae katuletea uzoefu wake kuhusu ATM zinavoweza ku misbehave na kufanya makosa kwenye kutoa fedha kwa mteja. Tena hapo ni bahati kwamba fedha zilikuwa zimezidishwa kwa mteja.

Kwa maana hiyo kuna uwezekano pia mashine hiyo hiyo ikafanya makosa na kumpunja mteja kwa kumpa kiasi pungufu ya alichodhamiria kutoa au kiasi sawa alichodhamiria kutoa lakini wakati huo huo risiti ikisoma kuwa fedha iliyotoka ni kubwa zaidi ya ile aliyopokea kwenye mashine. Na hii inaweza kuwaumiza zaidi wale wateja ambao mara nyingi uamini ATM na kuondoka bila kuhesabu fedha zao walizotoa.

Hivyo binafsi naona nimefaidika na post ya mchangiaji uliyemkosoa.
 
hahaha
 
kwani kuna tatizo dada? tuna share uzoefu
ila sawa nimekuelewa muungwana.
Na ulimbukeni mwingine wa kibongo bongo nao umekuandama... Kufikiri kumjibu mtu kwa kumwita ''dada'' ni ujanja! Tokeni kwenye ushamba uliwafunika ndugu zangu, dunia kubwa hii.
 
Umefaidika vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…