Wizi wa Magari ya Transit It

Wizi wa Magari ya Transit It

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
5,104
Reaction score
14,029
Recently Kuna majaribio mawili ya wizi wa Magari ya Transit yametokea katikati ya Iringa na Makambako jaribio la kwanza ni gari Toyota Mark X ambalo limefanikiwa na dereva bado yupo kituo cha polisi na jaribio la pili ni Toyota Landcruiser Prado hii mission ilikuwa failed hili lilitokea mchana ndio maana ikashindikana.

Nini kinatokea mamlaka zilipiga marufuku gari za IT kubeba abiria madereva wengi wa IT wameamia kwenye mizigo ili kuweza kupata pesa za ziada.

Wanachofanya wezi wa Magari ni kujifanya wanajeshi kwa kuvaa full sale za jeshi na kuomba lift kwenye gari za IT kuwa wanaelekea kambini makambako kwa makubaliono ya kulipa nauli madereva wengi wanachukulia kama advantage ya kuepuka usumbufu wa trafiki road.

Hawa wajomba wakifika sehemu za maporini wanaanza kukupiga na kukunyanganya gari kisha wanafunga plate namba za gari wanasepa

Hiyo ndio Mark X waliyofanikiwa kukimbia nayo
IMG-20260308-WA0004.jpg
 
Tanzania imerudi tena kwenye upumbavu haya mambo ya wizi yaliondoka kipindi Fulani.
Huu UJINGA ukiendelea baadhi ya nchi zitasitisha kutumia bandari ya DAR, madereva wa IT wanalipwa pesa kidogo Sana hii inasababisha waingie na tamaa ya kubeba abiria
 
Recently Kuna majaribio mawili ya wizi wa Magari ya Transit yametokea katikati ya Iringa na Makambako jaribio la kwanza ni gari Toyota Mark X ambalo limefanikiwa na dereva bado yupo kituo cha polisi na jaribio la pili ni Toyota Landcruiser Prado hii mission ilikuwa failed hili lilitokea mchana ndio maana ikashindikana.

Nini kinatokea mamlaka zilipiga marufuku gari za IT kubeba abiria madereva wengi wa IT wameamia kwenye mizigo ili kuweza kupata pesa za ziada.

Wanachofanya wezi wa Magari ni kujifanya wanajeshi kwa kuvaa full sale za jeshi na kuomba lift kwenye gari za IT kuwa wanaelekea kambini makambako kwa makubaliono ya kulipa nauli madereva wengi wanachukulia kama advantage ya kuepuka usumbufu wa trafiki road.

Hawa wajomba wakifika sehemu za maporini wanaanza kukupiga na kukunyanganya gari kisha wanafunga plate namba za gari wanasepa

Hiyo ndio Mark X waliyofanikiwa kukimbia nayo
View attachment 3564230

Ni kweli kabisa kwamba mazingira ya kazi ya madereva wa magari ya IT yanaweza kuwafanya waingie kwenye maamuzi ya hatari.

Malipo madogo ukilinganisha na umbali, muda wa safari pamoja na risk zinazohusiana na usafirishaji wa magari haya huwafanya baadhi yao kushawishika kubeba mizigo ya ziada ili kuongeza kipato.

Kitendo hiki kinapovunja utaratibu rasmi wa safari—ikiwemo route, muda na mfumo wa ufuatiliaji (tracking)—kinafungua mianya ya kiusalama ambayo inaweza kutumiwa na wahalifu, wakiwemo wanaojifanya vyombo vya ulinzi, kuvamia au kupora magari haya kwa urahisi.

Hivyo basi, kuna haja ya kuangalia upya mfumo wa malipo kwa madereva wa magari ya IT. Inawezekana kabisa kuwepo kwa viwango maalum vya malipo vitakavyopangwa na mamlaka husika, kulingana na aina ya gari na umbali wa safari—kwa mfano, gharama ya kusafirisha gari ndogo (saloon) kutoka Dar es Salaam hadi Tunduma iwe tofauti na ile ya magari makubwa kama SUV.

Malipo hayo yanapaswa kuakisi uhalisia wa kazi yenyewe—ikiwemo muda, uchovu, na hatari zote zinazoweza kujitokeza njiani—ili kupunguza kishawishi cha madereva kuingia kwenye ‘side deals’ ambazo hatimaye zinahatarisha usalama wa magari na mzigo kwa ujumla.
 
Utaratibu wa kupakia magari ya iT kwenye malori makubwa unaweza kuwa mzuri, hasa kama kukiwa na mlinzi msindikizaji anayekaa mbele na dereva kama abiria kumbe ana chuma cha moto
 
Back
Top Bottom