Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wizi wa magari hapa jijini na ukifuatilia kwa umakini kanda ya polisi Kinondoni ndiyo inayoongoza. Magari ambayo yamekuwa yakiibiwa kwa wingi ni aina ya Hiace, Coaster na Canter hasa hizi tani tatu zinazobinua. Wezi wa magari haya wamekuwa selective sana wa maeneo katika kufanya vitendo hivi wakijua hata ukienda kuripoti issue yako haiwezi kuwaathiri. Vituo vikuu vya polisi ambavyo vinahusika kwa namna moja ama nyingine ni kituo cha polisi cha Kawe na kituo cha polisi Magomeni, ukiibiwa gari yako na ukaripoti katika vituo hivi hesabu umeliwa. Wapelelezi wa vituo hivyo watakutoa hata milioni kadhaa za fedha wakidai wanawapa informer wao na kufuatilia mawasiliano ya wezi kutoka kampuni za simu lakini mwisho wa siku utaishia kukata tamaa pale unapoujua ukweli kwamba upelelezi haujafanyika na hata hayo mawasiliano ya simu hayajafanyika.
Kinachotokea ni kwamba polisi wa vituo hivi na hata wale wa kitengo cha wizi wa magari "Central Police" wanawajua kabisa wezi wa magari lakini watakukatisha tamaa katika upelelezi hadi utaamua kuacha ufuatiliaji. Kwa wale ambao ni wabishi katika kufuatilia na at least wana undugu na Polisi wa vyeo vya juu gari zao hupatikana mara baada ya kuuzwa kwa mtu (mara nyingi ni baada ya miezi 3 hadi 6) na si kutoka kwa wezi wa magari. Na ukiona gari limepatikana kwa muda mfupi basi ujue ni la mtu maarufu na anayejulikana serikalini.
Hata kama kwa bahati njema ukafanikiwa kumpata mshukiwa wa wizi wa gari yako, kwa kuwa wapo karibu sana na Polisi hasa wapelelezi wa kesi za magari watawekwa rumande kwa muda kukuridhisha na baada ya muda wataachiwa. Wakati mwingine hawawakamati kabisa hasa wale wanaohusika moja kwa moja, ni ngumu sana kupata haki yako Polisi endapo hujuani na bosi yeyote katika sekta hiyo. Ukitaka kujua usumbufu wa Polisi pata tatizo linalohitaji msaada wao!