SERGIO
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 348
- 145
Kumekuwepo na wimbi la wizi wa magari aina ya Noah ulioibuka hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Magari mawili yaliibiwa usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita kutoka eneo la maegesho katika nyumba ya mzee mmoja maarufu mitaa ya Kimara B Temboni. Taarifa zinasema walinzi wa Kimasai wanaolinda eneo hilo pia wametoweka na haijulikani waliko. Gari moja ni la mwenye nyumba na lingine ni la jirani yake aliyekuwa anaegesha hapo kwa malipo. Taarifa zilizopatikana jana zinasema magari mengine kadhaa aina ya Noah yameibiwa siku tatu zilizopita kutoka kwenye eneo la maegesho maeneo ya Kimara. Kuna dili gani inayohusisha magari haya?