Wizi wa kwenye simu

Wizi wa kwenye simu

sab

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2013
Posts
5,744
Reaction score
4,354
Habari waungwana wa humu jf.

Bila kupoteza muda nakwenda moja kwa moja kwenye mada,

Siku za hivi karibuni kumeibuka style ya wizi kwenye hizi airtel money , tigo pesa au m pesa, eazy money nk,

Utakuta mtu anakupigia simu nakujitambulisha kuwa ni mfanya kazi wa kampuni fulani ya simu hivyo anakupa maelezo ambayo moja kwa moja ni mbinu yakukuibia , sasa kwakua wewe hujui chochote unajikuta mwisho wa siku pesa zako zimekwenda kwenyr namba fulani ya simu ambayo namba zake amekupa huyo jamaa aliye jitambulisha kuwa ni mfanya kazi ya kambuni fulani ya simu ,

Baadae ya hapo unaamua kuwasiliana na kampuni yako ya siku kitengo cha huduma kwa wateja , unawaeleza issue ilivyo kuwa yote, wanakwambia pesa ulizo tuma zimesha tolewa na hawana uwezo wakukusaidia zaidi,

Sasa nauliza je hiii ni sahihi kweli ?
Inamaana hizi kampuni zinaendesha hii biashara bila bima ?
je hawawezi kujua pesa ambayo imeripotiwa kuibwa imetolewa kwenye kibanda gani na kipo wapi ?
 
Ndugu Yangu,
Hiki ni kipindi cha kuishi kwa akili sana.

Yaani mwili wako uulazimishe kuwa na akili nyingi kuliko damu yako.
Wizi Wa kila namna umekolea kwa sasa.
Viongozi wakubwa ndiyo wenye hiyo mitandao unayosema.
 
Inasikitisha sana kwakweli, mtu umejiwekea vijisent vyako alafu mtu anavikwapua na hupati msaada wowote
 
Inasikitisha sana kwakweli, mtu umejiwekea vijisent vyako alafu mtu anavikwapua na hupati msaada wowote
Pole sana mkubwa tena January hii ilivyo ngumu. Vumilia kaka hiyo ndiyo Elimu Dunia huipati shule.
 
Inasikitisha sana kwakweli, mtu umejiwekea vijisent vyako alafu mtu anavikwapua na hupati msaada wowote
Sab, niaje ndugu Yangu!

Wameshafanya yao watu wanaojifanya Wa mitandao?
 
Baadae ya hapo unaamua kuwasiliana na kampuni yako ya siku kitengo cha huduma kwa wateja , unawaeleza issue ilivyo kuwa yote, wanakwambia pesa ulizo tuma zimesha tolewa na hawana uwezo wakukusaidia zaidi,

Sasa nauliza je hiii ni sahihi kweli ?
Inamaana hizi kampuni zinaendesha hii biashara bila bima ?

Kuna kipindi walikuwa wanatangaza redioni kuwa kuna baraza la watumiaji wa mobile money waliishia wapi au nao walirudi kuungana na hao wezi baada ya kuona kupigania wahanga haiwalipi
 
Kinachowaponza watu wengi ni tamaa na si kingine, mara nyingi hudanganywa kuwa wamezawadiwa/wameshinda kiasi fulani (unashinda vipi bila kushiriki?! Huu ni upumbavu) hivyo ku-claim zawadi yako ndio hukupa maelekezo yao ya kitapeli.
 
Ni mazwazwa pekee wanatapeliwa kwa mtindo huo
 
Pole sana mkubwa tena January hii ilivyo ngumu. Vumilia kaka hiyo ndiyo Elimu Dunia huipati shule.
Actually , si mimi nimeibiwa, bali rafiki yangu
 
Sab, niaje ndugu Yangu!

Wameshafanya yao watu wanaojifanya Wa mitandao?
Fresh mtu wangu, sema sio mimi nijamaa yangu wamekwapulia kahela chake, alafu hakuwa na pesa nyingine, kwamekwangua yooote
 
Kuna kipindi walikuwa wanatangaza redioni kuwa kuna baraza la watumiaji wa mobile money waliishia wapi au nao walirudi kuungana na hao wezi baada ya kuona kupigania wahanga haiwalipi
Ndio nashangaa yaani , maana kama mtu anaiba alafu eti hakuna hatua yoyote yakuchukuliwa pamoja na taasisi zote hizi , ni shidaa
 
Kinachowaponza watu wengi ni tamaa na si kingine, mara nyingi hudanganywa kuwa wamezawadiwa/wameshinda kiasi fulani (unashinda vipi bila kushiriki?! Huu ni upumbavu) hivyo ku-claim zawadi yako ndio hukupa maelekezo yao ya kitapeli.
Ndugu, haya wajamaa wana style zaidi ya hizo ulizo mention hapo
 
Ni mazwazwa pekee wanatapeliwa kwa mtindo huo
Sawa mkuu, ila omba usipaywe ndio utajua, off course haijanikuta mimi bali rafiki yangu alafu sio rafiki mshamba mshamba au zwazwa kama unavyo sema, lakini aiku ya siku amepatikana
 
Lawama nyingine hazina maana kwani tatizo ni wewe mwenyewe kuendekeza tamaa na kupenda vya dezo.
Mkuu, wala sio style hiyo , mwanzo rafiki yangu aliponieleza ametapeliwa pesa zake nilifikiri hivyo kama wewe , lakini baada ya kunieleza kwa upana wake ndio nikaelewa haikiwa tamaa kama nilivyo dhania mimi, basi wakachukua vi sent vyake
 
Back
Top Bottom