Wizi wa kura bungen nani anahusika???

Wizi wa kura bungen nani anahusika???

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,787
Reaction score
37,992
Kama ni vituko nimeona leo ukishangaa ya musa utaona ya bungela katiba

katka kupata mwenyekiti wamuda kura zilihesabiwa zikakutwa zimeongezeka 20
tofauti na idadi ya wabunge

pengne kwa kuwa na mafara bungen ckushangaa wabunge wa ccm kupga kelele isirudiwe wengne wakicema kupoteza muda

maskini jaji warioba
marando akiweka wazi kuhusu katiba mpya amewapasha watanzania alichofanya raisi ni mchangawamacho

kilichotokeadodoma yale ndio maamuz yakatiba mpya akicema wakifika mwisho wataulizwa wanaokubali serikali 2 kidole!wanaoitaji serkal tatu kidole wengi wape katiba mpya inapita na kufanya mtikila na wenzake kuwj kama misukule pale bungeni
 
Ni wazi sasa uchaguzi wowote wa bunge tutapeleka wasimamizi ma kimataif

bunge licilo na.adabu wala aibu

mtoto wangu anaulza dady hzo nyingne zimetoka wapi nkamwambia zinaitwa maruhani
 
Ndivyo tulivyo ndivyo wanavyotuwakilisha
 
Inaonyesha jinsi utashi wa waTz ulivyo finyu. Ni aibu kwa chombo chenye wadhifa wa juu kabisa nchini kufanya kashfa mbaya kiasi hicho.
 
Hawa ccm wataiingiza nchi kwenye machafuko kama hawataacha kulazimisha mipango yao. Katiba imeitwa ya wananchi iweje wao ndo wawaamulie? Mkulu hebu akae na alowapeleka huko bungeni waache ubabe na waheshimu mawazo huru ya wengine bila ushabiki na itikadi zilizokwishapitwa na wakati kuepusha balaa lililo mbele yetu. Wasidhani watanzania ni maamuma wasiojua wanachokitaka!
Jk fanya maamuzi magumu vinginevyo tutaamini unataka kututawala badala ya kutuongoza.
 
Uhuni umefanyika kukwamisha katiba ya wananchi.
 
Lema keshawaombea Mwenyezi Mungu awatoe Uhai wao.... wasipo tenda haki...
 
Ndugu watz msitarajie maoni yenu kupita bungeni kama wameanza rafu, kwa ngazi za ungozi Wakati shughuli bado mbichi
 
Ccm hadi vikao vya chama kuteua wawakilishi wao wenyewe wanaiba kura, sembuse bungeni. Nilicheka siku moja walikuwa wanachagua mwenyekiti wao pale maeneo ya tabata bima, si wakaibiana wenyewe kwa wenyewe!
 
Kuna nahau inasema hivi, "ukitaka kuujua utajiri wa familia watazame watoto wanavyoonekana kwa kutokuvaa viraka". Hii inamaanisha kuwa busara na hekima ya baba huwaambukiza watoto automatically!
Kwa kinachofanyika kwenye bunge la katiba ni akiso la busara ya aliyewateua. Angekuwa makini pasi na misaha angewapeleka wateule makini wenye utashi , busara na hekima na si utoto unaoonekana huko! Ningekuwa mimi ndo yeye ningelivunjilia mbali kwa kuwa wamekosa sifa hata kabla mjadala hujaanza. Na hili limemchafua sana mwenye katiba magumashi mbele ya wakulu wenzie na huenda wanamng'ong'a kwa kushindwa kusimamia yale anayoyaanzisha. Labda aombe msaada wa wachina waje kumtengenezea katiba maana wateule wake wameshindwa kama walivyoshindwa kuwalinda tembo! Ni aibu kwa walimfahamu mwl. Nyerere kwa seriousness yake kwenye mambo ya msingi. Badilikeni bwana!
 
du!we kweli mnasihi.
 
Nyerere alimkataa huyu mtu mkamuona mjinga kazi mnayo miaka kumi mtaona kama mia kila alionalo mbele la kwake!Ktk mipango yake la katiba halikuwepo amefanya kulidandia baada ya kuona hana la kuja kuwaanbia watz kafanya!!!!!!
 
Wewe angalia wagombea walikua ni nani. Mahalu alikua na kesi ya wizi wa mamilioni ya pesa. Kificho kama jina lake sio muwazi na yule mama ni wa chechemaa. ulitegemea haki hapo ?
 
Mimi ambacho kimenishangaza sana ni mambo mawili: kwanza kutokujua idadi halisi ya wajumbe waliopo ukumbini na pili njia ya kupiga kura (manually, nasikia mjumbe mmoja alihoji kwa kuwa ni kura ya siri mbona hakuna mahala pa siri pa kupigia kura?). Yaani ukarabati woote wa mabilioni ya shilingi wameshindwa kuwa na mfumo wa kupiga kura electronically kila mtu abonyeze kitufe na kura ijiandike kwenye screen mbele wakati mjumbe akiwa amekaa kwenye kiti chake? Nasikia zoezi hili limechukua masaa sita kumchagua m/kiti wa muda, sasa siku ya Ijumaa (ambayo ratiba inasema ni uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu wake, maana huyu ni wa muda) si watatumia siku nzima?
 
Back
Top Bottom