Kumekuwa na mtindo wa wizi wa pikipiki kufanyikia huku maeneo ya Mbezi Beach. Mara nyingi abiria wanakodi pikipiki kutoka Kunduchi au Tegeta kuja Mbezi wakifika kwenye barabara za ndani ambazo hazina waenda kwa miguu au magari huwakaba madereva na kutokomea na pikipiki. Wizi hufanyika mchana na usiku hakuna muda maalumu.
Aina nyingine ya wizi hufanyika kwa abiria kukodi pikipiki akiingia tu maeneo ya Mbezi Beach pikipiki nyingine yenye abiria inaanza kuwafuatilia na wakifika eneo muafaka pikipiki ya nyuma inafanya kama inataka kuipita pikipiki ya mbele na abiria wake anaruka na panga, kisu, au bastola anawafuata.
Dereva wa bodaboda anapata vibao vya panga au anaambiwa uko chini ya ulinzi anaangushwa chini pikipiki hiyoo imekwenda.
Jana saa mbili na nusu usiku dereva wa bodaboda kaibiwa pikipiki mtaa wa Almasi kwa mtindo wa pikipiki mbili kufuatana! Madereva kuweni makini na wanaowakodisha!