Abbassalum
JF-Expert Member
- Dec 11, 2016
- 338
- 176
Alfajili ya leo saa kumi na ushee natokea kazini bandarini, nikapitia gate namba tatu, pale bandarini sasa wakati natoka pale gate namba tatu mkono wa kushoto kwangu kuna gari zile semi za bakhressa za kubeba ngano inapita inapeleka tazara pale kwa bakhressa, sasa mimi nipo nyuma ya ile gari, wakati naongozana nayo kufika kwenye ttraffic light za kamata, kumbe juu ya lile gari kuna vijana wawili, wakawa wanadondosha, viroba vya ngano kwa haraka haraka wakadondosha viroba kama, tisa vya ngano huku, gari likikata kona, kwa haraka wale vijana, wakashuka, kwa haraka pale kwenye karakana ya jiji pale nakumat super market, huku gari Ikiwa speed, sasa nikawa najuliza lakini jibu sijalipata, kama wale vijana, waliingiaje ingiaje, mule kwenye semi bila kuonekana na dereva au walinzi, au wanakula pamoja na madereva na walinzi ama inakuwaje hapo wakuu au hali ngumu ya uchumi, ndio maana wameamua wajitoe mhanga...!!!