wizi tigopesa

wizi tigopesa

Livia

Member
Joined
May 25, 2013
Posts
10
Reaction score
3
Wizi kwa mawakala wa tigopesa - Mwizi akamatwa

Tahadhari kwa mawakala wote wa Tigopesa

Wezi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa tigopesa wamekuwa wakiwaibia mawakala wa tigopesa kila kukicha. Wiki iliyopita maeneo ya Kimara mtu mmoja kwa Jina la Ally Abdallah alikamatwa baada ya kutoa pesa kwa kutuma msg hewa. Msg huoneka imetoka tigopesa kama kawaida ila inakuwa na makosa mengi ikiwepo number ya simu ambao wanakutumia namba yako ya uwakala, pamoja na tarehe feki na salio feki. Mtu huyu kwa Jina la Ally Abdallah ni hatari sana na ameiba sehemu nyingi kama dodoma na kwingineko. Ukitafuta kwenye mtandao utamkuta ila inaonekana kote amefanikiwa kuachia na police. Mwezi huu aliiba maeneo ya Kimara na akakamatwa na kupewa mkong'oto wa kufa mtu. Alipotaka kuchomwa moto wasamaria wema walimtetea asiuwahe. Na alipopelekwa kituo kidogo cha police Kimara - wanamtandao wenzako walienda kumchomoa haraka na sasa ametoweka. Sijui rushwa itaisha lini police. Picha za kitambulisho chake hiki hapa. Kuweni makini huyu jamaa ni hatari sana. Anashirikiana na wafanyakazi wa tigo kuiba. View attachment 95061

 
Wafanyakazi wa tigo sii waaminifu hata chembe,mwaka jana walifukuzwa 30 upande wa IT
 
Wahindi wanawapasua mishahara kiduchu sana ndo maana ni wezi sana ktk mitandao yote tigo ndo wafanya kazi wake choka mbaya hawana tofauti na walimu na bado watatupasua sana hao jamaa
 
Back
Top Bottom