Wizi mpya umeibuka...kaa chonjo

Majuzi tulijadili kuhusu mtunzi wa riwaya wa kimataifa unayemkubali. Hapo ndio namkubali marehemu Sydney Sheldon. Kama umesoma novel yake ya "IF TOMMOROW COMES"huwezi ukatapeliwa kwa mtindo huo. Kitabu hicho japo ni cha miaka ya tisini au kabla kina mifano kadhaa kama hiyo. Ili usitapeliwe inabidi usiwe na tamaa. Kazi ya tapeli ni kukutia tamaa. Ukiishinda tamaa umemshinda tapeli. Soma riwaya hiyo upate maarifa ya kushindana na matapeli wa aina hiyo.
 
Mim nawashangaa mnaomsema eti kuwa ametunga haijamtokea bali amekopi story ya miaka ya nyuma, mimi sioni ana sababu gani ya kufanya hivyo na pia sioni nyie mna sababu gani ya kutomuamini............anapata faida gani akiwadanganya? Mimi nadhani ni kweli imemtokea....Shaycas, kuhusu vyombo vya dola kutoa taarifa ya utapeli huu mmh nina imani wanajua na wala sijawahi kusikia wakitangaza, sitashangaa kuwa na wao (vyombo vya dola) wanashirikiana nao....... THIS IS BONGO BAAANA
 
Dah dah dah! Pole sana mie niliokolewa na michuzi blog hbr hii inaandikwa sana kule michuzi blog!Walinipigia, wacha niwasanifu namba zao zoye wanazotumia ninazo bahati mbaya tu sikupata ushirikiano wa polisi kuwanasa!But tumeapa wakiingia line kwa mtu wa krb yangu awatege tuwakone tubonde wenywe kipigo cha mbwa mwizi!Na kweli cku si siku akapigiwa rafiki yangu wakaribu, amekwenda nao kila akiwambia waje town hawataki wanadai mshikaji aende sinza, tukaachana naoBut pole sana ndugu
 
Kaka nilivyoanza kusoma story yako mwanzoni tu,nkajua nini kingefuatia,biashara kubwa km hyo lazma ingekuwa na restriction za hapa na pale,ww hukuingiwa na wasi wasi??
All in all pole sana!!
 
Hata kama ni "copy and paste" ni habari nzuri, tuendelee kuhabarishana.
 
watu wana akili! Dah, hapa naona wamekuonea huruma, 1m ni kidogo mno, kwa jinsi ulivyokuwa na wenge la utajiri hata kama ungeambiwa 10m ungeona cha mtoto. Pole sana.
 
teheeeeeeee, teheeeeeeee
,..wat kind of personification is this?
 
Pole sana ndugu ndio nchi yenyewe pesa inatafutwa kwa kila njia. Tuwe waangalifu.
 
Pole mkuu, mimi pia ilisha nitokea mara mbili, mwaka juzi mara moja bahati nilikua nimesha tumiwa e-mail na one of my friends.
Tapeli alivonipigia cm exactly aliongea kama ile e-mail ilivyohadithia kwa hiyo nilimwambia tapeli huyo anipe muda nimalize kazi then tutaongea, nikiwa natafuta njia ya kumkamata, but badae nikaaachana nae na alinisumbua sana kwa sim sikupoke.

Last month tena nimepigiwa sim nikatajwa jina na ubini pia, tapeli huyo akaongea maneno hayo hayo, na sikuzote huwa wanadai wanafanya kazi WFP, then nikamwambia mimi pia niko WFP mbona sikufaham na hakuna biashara kama hiyo? akadai ooh mi niko UN kigoma.
Nikamgombeza sana nikamwambia ukiendelea utaishia kufungwa utapeli wako hautakusaidia, akaniambia kwahiyo umekataa business nikamjibu ndiyo nimekataa na ukiendelea ntakufunga.

Nimegundua hawa watu wanapata contact kwenye bsns card za watu na ndo wanazozitumia bila hata kujali na ndio maana hua wanaanza kwakusema bado uko office flani.
TNikweli tunatakiwa kulijua hili kwani lipo.
 
utapeli wa kizamani sana mkuuu zamaani sana mkuu
 
Pole sana, kila siku kuna mbinu mpya ya kufanya mkono uende kinywani hata kama ni haramu.
 
Pole sana ndugu yangu,
Huu utapeli haujitokezi sasa kwa mara ya kwanza. Ninachokuomba ni kuwa unaweza kufuatilia kupitia polisi, Makampuni ya simu na TCRA ili upate hela zako. Unless hizo namba hazijasajiliwa na TCRA wamefanya utapeli wa kutuambia tusajili huku wakijua kuwa hawakuwa makini na zoezi lao lakini wanawajibika 100% kujua wenye namba na mahali walipo.

Aidha napenda kutahadharisha watanzania wenzangu kuwa macho na fedha za chapchap. Ukitaka utajiri wa chapchap unaweza kuambulia hasara ya chapchap!
 
Kuna ndugu yangu mmoja bado kidogo alizwe kilichomsaidia baada ya kupata iyo dil aliwashirikisha jamaa zake wakamtonya kwamba hao ni matapel
 
umeniacha hoi pale ulipochukua calculator ya sim, dar zero zero zikazid mpaka ikagoma, kwel imani huja kwa kusikia, unapompa m2 chans ya kumsikiliza wakat humjui hapo ndo shda inapoanza
 
Duh ,pole sana mkuu
nina imani hata mimi ningeweza kuingia.
Ninashukuru kwa taarifa
 
Tunashukuru sana kwa kutuzindua! Vile vile kuna matapeli wanaotuma emails kutapeli watu. Watakuambia umeshinda bahati nasibu au kuna kibunda cha urithi cha kugawana n.k. Tusitake utajiri wa bila jasho una cost yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…