Wizi huu mpaka lini???

Fisherscom

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
1,763
764
Jana nilikuwa safarini toka Dar kuelekea Mbeya kwa kutumia usafiri wa mojawapo ya basi la kampuni kubwa hapa nchini. Safari yetu ilikuwa nzuri toka Dar asubuhi hadi mida ya mchana saa saba tulishuka Ruaha Mbuyuni eneo la Al Jazeera kununua vyakula pamoja na kuchimba dawa. Abiria wote walishuka ndani ya gari kondakta anadai alibaki garini mlangoni kuangalia usalama wa basi lile. Tuliporejea ndani ya basi abiria wawili walidai kutoziona laptop zao pamoja na simu zao mbili. Taarifa zilifikishwa kwa dereva nae akashauri tuendelee na safari hadi Ilula ambako kuna kituo cha polisi. Tulifika Ilula na ukaguzi kufanyika ndani ya gari na nje kwenye eneo la mizigo. Hadi mwisho wa zoezi hilo hakuna kilichopatikana na kuthibitisha vitu hivyo kuibiwa. Muda uliopotea safarini kutokana na wizi huo ni zaidi ya masaa mawili na kupelekea kufika Mbeya saa 3.30 usiku.
Swali langu ni kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri pamoja na wahudumu + madereva wamejiandaa vipi/wanalichukuliaje tatizo kama hilo?
Pia wasafiri wanajiandaa vipi kukabiliana na matukio kama hayo ikiwa dhamana ya usalama wa mali zao ipo kwa wahudumu na wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri?
 
Mkuu kama unataka jibu la swali lako, wizi huu utaendelea mpaka siku serikali itakapokuwa serious. Kama angeibiwa kiongozi wa serikali waziri na waziri mkuu hizo laptop zingepatikana. Kungekuwa na utaratibu wa kuyafutia leseni magari ambayo hayahakikishi usalama wa mali za abiria, hiyo ni hatua moja ambayo serikali inawezam kuchukua.
 
asante sana kwa taarifa mkuu lakini huoni kama na wewe unaendeleza hili tatizo kwa kuogopa kutaja jina la basi/kampuni ambalo tukio hili limetokea? ukitaja jina la basi utawasaidia wasafiri wengine wakae nalo mbali au tuwe makini kwani aliyebaki ni konda peke yake kulinda mizigo ya watu.
 
ahsante mkuu,swali hilo nilitambua litakuja nilikuwa nasubiri nguvu ya great thinkers. Ni basi la Sumry la saa 12.45 asubuhi Dar-Mbeya.
 
Hata mimi nilitaka kuuliza....wewe utaachaje laptop kwenye basi? Hata majuu kwenyewe watu hawaachi laptop hovyohovyo namna hiyo.
 
......ilikuwaje mwende ILULA wakati pale Mbuyuni kuna Kituo? Huoni hapa ndipo ulipoiicha Laptop yako Ruaha Mbuyuni?
 
Hilo ni kosa lilifanyika na mjadala mkali ulifanyika ndani ya basi na polisi Ilula walizungumza hivyo ila ni kiburi cha dereva kuangalia zaidi anakoelekea wakati upekuzi huo ungeweza kufanyika Ruaha.
 
mkuu,hata ukiacha hachukui mtu sanasana wataitwa ANTI-TERROR SQUAD au BOMB DISPOSAL UNIT......
Point ni kwamba pamoja na ulinzi na umakini uliopo pale, siezi kumuachia mtu laptop yangu ambayo ni kama my best friend kwene sayari hii. I would n't trust anyone with that.
 
Jana nilikuwa safarini toka Dar kuelekea Mbeya kwa kutumia usafiri wa mojawapo ya basi la kampuni kubwa hapa nchini. Safari yetu ilikuwa nzuri toka Dar asubuhi hadi mida ya mchana saa saba tulishuka Ruaha Mbuyuni eneo la Al Jazeera kununua vyakula pamoja na kuchimba dawa. Abiria wote walishuka ndani ya gari kondakta anadai alibaki garini mlangoni kuangalia usalama wa basi lile. Tuliporejea ndani ya basi abiria wawili walidai kutoziona laptop zao pamoja na simu zao mbili. Taarifa zilifikishwa kwa dereva nae akashauri tuendelee na safari hadi Ilula ambako kuna kituo cha polisi. Tulifika Ilula na ukaguzi kufanyika ndani ya gari na nje kwenye eneo la mizigo. Hadi mwisho wa zoezi hilo hakuna kilichopatikana na kuthibitisha vitu hivyo kuibiwa. Muda uliopotea safarini kutokana na wizi huo ni zaidi ya masaa mawili na kupelekea kufika Mbeya saa 3.30 usiku.
Swali langu ni kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri pamoja na wahudumu + madereva wamejiandaa vipi/wanalichukuliaje tatizo kama hilo?
Pia wasafiri wanajiandaa vipi kukabiliana na matukio kama hayo ikiwa dhamana ya usalama wa mali zao ipo kwa wahudumu na wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri?

mimi nadhani hao abiria ni wazembe, na ni nani alihakikisha kuwa kweli walikuwa na laptop na simu?...je kama ilikuwa ni njama ya kuchunguza ni nani na nani wana nini na nini ili waibe au hata mkifika huko mnakokwenda (maana mlifika usiku) wawavizie wawakabe na mwisho wawaibie....ni mtazamo wangu tu lakini
 
Hao wenye basi ndo walioiba hivyo vitu. Lakini pia kuna ujumbe karibu kila basi unasema: "Abiria chunga mzigo wako". Ni jukumu la msafiri pia kutambua vitu vya thamani ambavyo umebeba kwenye beji lako na kujitahidi kuvilinda wewe mwenyewe bila kuamini mtu yeyote mwingine. Shida yetu wabongo: tunaaminiana kirahisi sana na wakati mwingine kuchukulia mambo kirahisi tu kwamba hakuna baya linaloweza kutokea. Hili liwe ni somo kwa wasafiri wote. Ila pia wahudumu wa basi hilo lazima wawe si waaminifu. Yawezekana ndo waliotenda unyama huo.
 
Mimi huwa nasafiri saana na hayo mabasi pamoja na new force na mara nyingi huwa nasafiri kikazi.Hivyo japo huwa wanatangaza kuwa Kondakta atabaki ila cjawahi kuacha laptop yangu ndani ,huwa natoka nayo.Anayeingia hasara c mwenye gari bali ni wewe.Na hiyo hasara ni kubwwa maana unapoteza documents nyingi saana.Kuweni makini abiria-msiamini kila mtangaziwacho muwapo safarini hasa kuhusiana na usalama wa mizigo yenu
 
jamani watu 65 wote walishuka? huwa mara nyingi kunakuwa na movement za hapa na pale bana! vile vile kwenye tiket kumeandikwa mzigo wa ndani ya basi sio dhamana yetu nadhani, au!!!!!???
 
Inawezekena hiyo mobile na laptop abiria hakununua kwa pesa yake. kama alinunua kwa pesa yake basi hivyo vitu thamani yake kwake ni kama kandambili. Sio rahisi kuwa mzembe kiasi hicho.

Na kama alivyosema moa mada 1ja kutotaja jina la basi kunazidi kutia shaka uhakika wa habari yenyewe. Taja jina la kampuni uwasaidie watu.
 
Jana nilikuwa safarini toka Dar kuelekea Mbeya kwa kutumia usafiri wa mojawapo ya basi la kampuni kubwa hapa nchini. Safari yetu ilikuwa nzuri toka Dar asubuhi hadi mida ya mchana saa saba tulishuka Ruaha Mbuyuni eneo la Al Jazeera kununua vyakula pamoja na kuchimba dawa. Abiria wote walishuka ndani ya gari kondakta anadai alibaki garini mlangoni kuangalia usalama wa basi lile. Tuliporejea ndani ya basi abiria wawili walidai kutoziona laptop zao pamoja na simu zao mbili. Taarifa zilifikishwa kwa dereva nae akashauri tuendelee na safari hadi Ilula ambako kuna kituo cha polisi. Tulifika Ilula na ukaguzi kufanyika ndani ya gari na nje kwenye eneo la mizigo. Hadi mwisho wa zoezi hilo hakuna kilichopatikana na kuthibitisha vitu hivyo kuibiwa. Muda uliopotea safarini kutokana na wizi huo ni zaidi ya masaa mawili na kupelekea kufika Mbeya saa 3.30 usiku.
Swali langu ni kwa wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri pamoja na wahudumu + madereva wamejiandaa vipi/wanalichukuliaje tatizo kama hilo?
Pia wasafiri wanajiandaa vipi kukabiliana na matukio kama hayo ikiwa dhamana ya usalama wa mali zao ipo kwa wahudumu na wamiliki wa vyombo hivi vya usafiri
?

Mkuu, mbona unakua kama mgeni wa bongo??? Umesahau "ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO??

Hivi kweli mtu anayethamini laptop na simu anaweza kuacha hivyo vitu kwenye gari lenye strangers zaidi ya 40???

Careless!!!!!
 
afadhali laptop i can understand...
jamani simu i thought is one item kila mahali uwe nayo!!
au wenzangu wamesahau matumizi ya simu...??
huu ni uzembe wa hali ya juu
 
Back
Top Bottom