Wizara ziwe hivi

samaki hawana vizara kwenye serikali yako... vipi kuhusu wanawake... wasio na wizara maalum je?

Samaki...... mmmmh! nadhani hao pia wanafugwa so ni mifugo..

Wiraza nyingi zinaaccelerate ufisadi kama ilivyo school..group discussion ikiwa na watu wengi... mnatoboa kwa story!
 
Kuunda wizara inahitaji umakini na utulivu wa hali ya juu wa wataalam watakaozingatia mambo mengi kabla ya kuamua. Haitaki kukurupuka tu na kutengeneza list.

Wataalamu ni akina nani? This is pure status quo talk, kila siku tunaambiwa wataalam wanafanya upembuzi yakinifu kwa hiki na kile, na mbona kama wamepanga kwa umakini, hatuoni umakini wake katika kutimiza majukumu yao?
Umakini ni pamoja na kupunguza gharama, kama wizara kumi zikipunguzwa, na kila wizara ina mashangingi walau 10, [ waziri, naibu, katibu mkuu, na naibu wake, wakurugenzi, meneja mradi n ,k] kila shangingi ni milioni 100, [ kwa bei wanayoitaja wao ] na mafuta milioni mbili kila mwezi, je ni kiasi gani tutaokoa? na hapo ni gharama za magari tu.
 
Ni kweli kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na Wizara chache iwezekanavyo, ambazo zinaweza kuleta tija zaidi. Ila ninavyoamini ni kwamba, sekta nyingi zinahitaji kupewa wizara zake kutegemea na vipaumbele vilivyopo.

List hiyo hapo juu inaweza ikawa nzuri kwa serikali ambayo ina malengo fulani. Na pia inaweza ikawa haina tija kama haikuzingatia priorities zilizopo. Inaweza ikawa ni serikali ambayo inakwenda tu ili siku ziende bila kutegemea jipya.

Ukubwa wa serikali kama ilivyokuwa serikali ya kwanza kabisa katika awamu hii, pia haimaanishi kuwa utendaji utaongezeka.

Mix ya muda wa kufikia malengo muhimu, gharama ya kufikia malengo hayo na ubora wa malengo yanayotakiwa kufikiwa ndio inayotakiwa kuamua ni aina gani ya serikali, watu na resources nyinginezo zinazohitajika kuunda serikali. Mara nyingi haya hayafanyiki, badala yake viongozi hupatikana kutegemea na ushiriki wa mtu katika kuhakikisha chama kinashinda uchaguzi, ama nguvu walizonazo kwa umma n.k. Labda ndio maana tupo hapa tulipo, ambapo kitu pekee tunachojaribu kujivunia nacho ni amani, umoja, utulivu na uzalendo (ambavyo ukitaka kuviachambua, wala pia havipo).
 
Back
Top Bottom