Wizara ya Waziri Magufuli hoi kifedha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Waziri Magufuli hoi kifedha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Mar 30, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Imebainika kuwa chanzo cha miradi mingi ya barabara nchini kukwama kumalizika kwa kipindi kilichopangwa inatokana na madeni inayodaiwa Wizara ya Ujenzi, Sh. bilioni 331 kutoka kwa makandarasi hadi Februari, 2012.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, John Cheyo, alisema mwisho wa mwaka 2009-2010 Wizara ya Ujenzi ilikuwa na madeni ya Sh. bilioni 44 na hadi kufikia Juni 30,2011 madeni yaliongezeka mpaka Sh. bilioni 420. Aliongeza kuwa kufikia Februari 30, 2012 Wizara ya Ujenzi ilipokea Sh. bilioni bilioni 384 kutoka Hazina ambayo ni pungufu ya madeni inayodaiwa.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Herbert Mrango, alisema wizara hiyo haipati fedha katika muda mwafaka kutoka Serikalini, ila wamehaidiwa kupewa Sh. bilioni 317 na Serikali kulipa madeni hayo.

  Akitaja miradi ambayo imesitishwa kuendelea kutokana na wakandarasi kuidai Wizara ya Ujenzi, Cheyo ni barabara kutoka Bariadi kwenda Lamadi, Ndundu kwenda Somanga yenye urefu wa kilomita 60, iliyogharimu Sh. bilioni 58.8 na Wizara imeshalipa Sh. bilioni 46 na kudaiwa Sh. bilioni 12.

  Nipashe
   
 2. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  biashara ifanyikayo hapo ni tunakupa advance then anza kazi na ukifikia hatua fulani tunakupa 2nd advance. kwa kifupi ni biashara ya mkopo.
   
 3. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  au hukutaka wizara ikope??
   
 4. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Maswala ya Mahusiano ya Kifedha kati ya serikali na organ yoyote isiyo yakiserikali yako chini ya wizara ya Fedha, hakuna wizara inayoruhusiwa kukopa wala kukopesha pesa hovyo hovyo. Msituendeshee hii nchi kama vichaa jamani.

  Kama mnataka kabadirisheni taratibu za usimamizi wa fedha si mnayo madaraka, hata taratibu mnazoweka wenyewe hamuwezi kuzisimamia watu wanamna gani nyie?
   
 5. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Halafu ni huyu Magufuli alikuwa anajitamba kwenye ufunguzi wa barabara moja kama sikusei ni Manyoni vile eti wanaobeza serikali juu ya ujenzi wa mabarabara tena kwa fedha zetu wenyewe ni wajinga!!!

  Watu walikuwa wanamshangaa lakini walimsamhe kwa sababu ni mwanasiasa tena kutoka CCM!!!!

  Ona sera za CCM!!!!!!!!!
  Nipigeeeeeeee Nisipigeeeeeeee??????????????? ?????
  Pigaaaaaaaaaaaa
  Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii????????????? ??
  Kijaniiiiiiiiiiiiii.
  Ukipanda mahindi yanaota rangi ganiiiiiiiiiiiii???????????
  Kijaniiiiiiiiiiiiii.
  Ukipanda mpunga unaota rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????
  Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
  Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?????????????
  Kijaniiiiiiiii.
  Piga makofi na vigelegele kwa Chama cha Mapinduzi.
  CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeeee.
  Oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
   
Loading...