Wizara ya Viwanda na Biashara, inabidi muangalie namna ya kuongeza viwanda vya kutengeneza meli na boti (Ship and Boat Builders) nchini

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,952
12,528
Kwa kipindi kirefu Tanzania tumekuwa na kiwanda kimoja au sehemu ya kutengenezea meli na boti ambayo inamilikiwa mzawa Songoro Marine and Boat yard.

Wizara ya viwanda na Biashara inabidi iangalie namna ya kuwashawishi watengenezaji wengine nje ya nchi au kuwapa hamasa wazawa kuanzisha viwanda hivi.

Wizara ifanye mazungumzo na balozi au kwenda kwenye nchi mashuhuri kwa kutengeneza meli na boti kama Japan, Korea Kusini, China, Ugiriki na Norway na kuongea na wamiliki wa Ship yard kuja kuwekeza hata kwa ubia nchini kwetu.

Songoro amefanya project nyingi hapa nchini anastahili pongezi, lakini ili tufike mbali zaidi inabidi kuwe na washindani ili tuone teknolojia za kisasa na ubora zaidi.

Tanzania tuitumie vyema bahari ndio mgodi usio na mwisho.

SEA NEVER DRY
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom