Wizara ya viwanda itizame hii changamoto SIDO inavyokwamisha ustawi wa viwanda

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Kwa sasa serikali iko kwenye mkakati wakuanzisha viwanda nchini hili ni wazo zuri na kama litasimamiwa ipasavyo litatuvusha.

Hatuwezi kuzungumza habar ya viwanda bila kuigusa hii taasisi muhimu ambayo kwa sasa ipo taabani ukilinganisha na miaka ya nyuma.

Sido inakitengo cha mikopo kwa wajasiriamali wenye viwanda na kwakweli riba yake ni nafuu sana kwani 10% tu ya mkopo.

Ukiachilia mbali riba ndogo lakini SIDO pia inavigezo wezishi kwa wajasiriamali wanaohitaji kukopa kwani wanakubali hata dhamana za hati zakimila za mashamba/viwanja ama hati za vijiji.

Lakini changamoto kubwa kima cha juu kabisa kwa sasa cha mkopo ni tsh 2,500,000 tu pesa ambayo ni kidogo mno kama kweli tuko serious na mkakati wa viwanda.

Ukitizama budget ya mh Charles Mwijage ni 80 bilioni pekee pesa ambayo ni vigumu kuona mafanikio kama itaongozwa kwenye uwekezaji wa viwanda vikubwa kwani haitotosha.

Nilimsikiliza mh Bashe jana amesema tathimini iliofanyika ili kufufua kiwanda cha general tyre tunahitaji 60 bilion unaweza ona ugumu ulivyo ukilinganisha na budget ya wizara.

Lakini taasisi kama SIDO kama inaweza kutizamwa vizuri viwanda vidogo havihitaji uwekezaji wenye kuhitaji pesa nyingi lakini vinaweza kuajiri vijana wengi na serikali ikapata mapato pia.

Ila kwa sasa ukitembelea ofisi za SIDO ni kama zimekufa hata vile vipeperushi mnavyoona SIDO wakionesha mashine mbalimbali ama kipindi cha maonesho ya sabasaba zinatoka kwenye karakana za wajasiriamali binafsi na sio sido kama taasisi.

Hivyo ni vema hii taasisi ingesukwaaupya kwani zamani SIDO walikua wakifanya vizuri sana.
 
Back
Top Bottom