Wizara ya Uhamiaji na watu wa idara ya kazi njooni Kibaha

manSniper

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
814
679
Nimeona suala la Waziri wa Mambo ya Ndani alilotoa kwa idara ya uhamiaji kuchunguza vibali vya wafanyakaz wa nje kufanya kazi Tanzania, kuna mradi wa maji unaoendela Ruvu juu mpaka Dar amepewa contractor toka India yaani kaleta wahindi tupu yaani vibarua, maoparetor, mafundi, wapishi, madereva wachimba mitaro, walinzi wote toka India ni wengi wanaishi maeneo ya hapa Ikunda gesti. Pale wapo zaidi ya mia hapa Maili Moja, sasa nauliza hizi shughuli si zilikuwa ni za wazawa?

Vijana hawana ajira hapa Maili Moja, Picha ya Ndege kwa Mathias,Kongowe, Mlandizi. Sasa kuwaleta hawa wahindi wanalipwa shi ngapi kuwalisha na kuwalaza?

Ukienda kuomba kazi unaambiwa per day 10000, hebu idara ya uhamiaji na idara ya kazi ifuatilie ofisi zao zipo idara ya maji karibu na stendi Mail Moja hapo.

Saidieni kwa hili tafadhal sana haraka hili bomu la ajira limelipuka huku kumezidi wizi vijana hawana kazi wahindi wameiba ajira zetu, mbunge Koka hamna kitu anafuatilia zaidi ya tenda yake ya kupika bungeni.
 
Uhamiaji Ni Jipu
Huko Rais Anatakiwa Kwenda Kupakamua Kwanza
Halafu Mambo Yaende Vema
 
Waende Mikocheni Industrial area kuna wahindi hadi wafagizi.
Waje Posta kuna wapishi na mawaiter wa kihindi kibao.
Waende Mbozi na Pugu Road kuna wahindi kibao wanafanya kazi za kawaida kabisa
 
Ukipenda kuomba masharti lazima yazingatiwe , hiyo ni sehemu ya package ya msaada,hiyo ni kawaida kwa nchi masikini kupewa masharti.
 
Huo mradi ni wa MSAADA. Tanzania imepewa msaada wa $180 million na India mwaka 2011 kusaidia watu wapate mahitaji ya maji. Pia, imekopeshwa $380 millioni katika sekta hiyo hiyo.

Sasa, ukiomba msaada, ni standard kwa nchi inayotoa msaada kuleta watu wake ili walipa kodi hiyo kwao wapate kazi na tenda.
Wachina walileta watu wao kujenga Tazara vile vile.

Pia, mtoa mada, una uhakika kama Tanzania kuna wataalamu wote wanaohitajika katika hiyo kazi?

Serikali ya India pia imetoa msaada mwingine wa $10 milioni kuboresha elimu yetu na $150 milioni kujenga hospitali ya upasuaji wa moyo.

Mhindi mbaya, kiatu chake dawa!



Source:

DAR ES SALAAM (Reuters) - India said on Friday it would give Tanzania $180 million to upgrade water supplies in the East African nation, and the two countries agreed to remove tax hurdles and boost bilateral trade.
New Delhi earmarked a further $10 million of aid for the education sector.
The two countries also signed a deal for the construction of a $150 million hospital specialising in heart surgery in Dar es Salaam.




 
Back
Top Bottom