WIZARA YA NISHATI

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Leo tarehe 04/10/2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, anafanya ziara katika eneo la mradi wa umeme wa Rufiji (2100) ambapo atakagua utekelezaji wa miundombinu wezeshi ya mradi huo ikiwemo ujenzi wa barabara, miundombinu ya umeme, kituo cha reli kitakachotumika kushushia mizigo na miundombinu ya maji.

Katika ziara hiyo, Mhe Waziri Mkuu atapata taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.

Waziri Mkuu anaambatana na Mawaziri mbalimbali wanaohusika na mradi huo na watendaji wa Wizara na Taasisi zinazohusika na mradi tajwa.

Kutoka Wizara ya Nishati, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Eng. Innocent Luoga anashiriki ziara hiyo ambapo pia anamwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
 
Back
Top Bottom