Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuja sheria kali ya uvuvi haramu

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
Tanga. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema wapo katika hatua za mwisho ya kuandaa mapitio ya Sheria ya Uvuvi itakayokuwa na adhabu kali kwa watu watakaobainika kufanya uvuvi haramu.

Katika sheria hiyo imependekeza watu watakaobainika na kuthibitika kufanya uvuvi haramu wahesabike kama wahujumu uchumi na wataadhibiwa kulingana na makosa ya uhujumu uchumi.

Ulega ameeleza hayo leo Alhamisi Oktoba 26 wakati akipokea ripoti ya hali ya uvuvi na ufugaji katika Mkoa wa Tanga.

Ulega amesema wapo katika hatua nzuri katika kuandaa mapitio ya sheria hiyo na kwamba, baada ya kukamilika wataipeleka bungeni kwa ajili ya kupata ridhaa ya wabunge.

Amesema bado kumekuwa na changamoto katika uvuvi hali inayohatarisha mazalia ya samaki.

"Sheria hii haitamwacha mtu salama endapo atathibitika kufanya uvuvi haramu wa kutumia nyavu zisizo na vigezo au kutumia mabomu. Tutashukuru sana wabunge watairidhia ili kuilinda sekta ya uvuvi na kulinda rasilimali za bahari, mito na maziwa," amesema Ulega.

Ulega amesema mamlaka husika itafanya doria mara kwa mara ya kupambana na uvuvi haramu lakini sheria hiyo itakuwa ni mwarobani ya kuthibiti tatizo hilo.

Amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela kwa kazi nzuri anayoifanya ya kudhibiti uvuvi haramu na sanjari na kuhakikisha sekta ya mifugo inapiga hatua.

Awali, Shigela alimweleza Ulega kwamba mkoa huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti uvuvi wa kutumia mabomu baada ya kufanya doria ya mara kwa mara kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama.


Mwananchi
 
Sheria iliyopo sasa inaonekana kama ni "rafiki" kwa wavuvi haramu eeh... Basi acha tu adhabu iongezwe
 
Back
Top Bottom