Wizara ya mifugo inafahamu haya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya mifugo inafahamu haya?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hofstede, Feb 7, 2009.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli usiopingika kuwa wafugaji wetu ni muhimu sana katika kutuhakikishia kuwa tunajitosheleza kwa mazao ya mifugo kama, nyama, ngozi na maziwa. Ingekuwa ni busara zaidi kwa wizara ya mifugo kuwaelimisha wafugaji wetu namna ya kuwa na mifugo bora bila kuharibu mazingira kwani kitendo kinachofanywa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa hakiendani na dhana nzima ya kuwaendeleza wafugaji bali ni kuwafilisi na kuwafanya waachane shughuli hii ya kutupatia nyama na mazao mengine. Je hawa wafugaji wakiachana na ufugaji serikali inaweza kufanya kazi inayofanywa na watanzania hawa wasio na elimu na kuadhibiwa kwa kutokuwa na ufahamu?.

  soma habari hii ili uone unyanyasaji wanaofanyiwa wafugaji wazalendo katika nchi yao huru chini ya serikali yao walioichagua kwa kishindo ili kuendelea kuwatetea.
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii yote inatokana na kutokuwa na mipango endelevu. Vipi utawasaidia wafugaji wafuge kisasa na wakati huohuo wasiingie katika maeneo ya kilimo. Manake zote hizi mbili (ufugaji na kilimo) ni shughuli za maendeleo. Wafugaji wanapigana mpaka kuuana na wakulima siku hizi, sababu wanagombea maeneo, wafugaji wanalisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima. Hivyo lazima kuwepo taratibu za kuwawezesha wote kuendesha shughuli zao bila kuathiriana.

  Pole mfugaji Dotto Duffu manake japo umelipa hiyo faini, wanao wanne wamepotelea porini. Hapa Serikali inatakiwa kumsaidia kuwatafuta manake wao ndio chanzo cha hao watoto kukimbia na kupotelea porini.
   
 3. e

  eddy JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,361
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Kama ndo hivi basi tutegemee akina nkunda kupatikana sio muda mrefu! naimani wasukuma hawa kuna siku watasema sasa imetosha.
   
Loading...