Wizara ya michezo inaendesha Semina ya Kibaguzi Mwanga Kilimanjaro

kibacha

Member
Nov 14, 2013
50
26
Wakuu,

Muda huu ninaoandika hapa, serikali kupitia wizara ya michezo inaendesha semina ya kibaguzi hapa Mwanga Kwakuwaita vijana waccm pekee kwenye semina wanaodai ni yakuwajengea vijana uwezo wa kukopa na kurudisha, semina hii ilianza jana tarehe 08.01.2015 kwenye ukumbi wa viziwi huku bomani.

Wengi wetu hatujarudi leo kutokana na posho ya siku kuwa ndogo yaani tunalipwa ELFU 5000 huku tukiambiwa tusaini ila tusiandike kiwango hivyo sehee ya Amount inabaki wazi Tsh........................ then mbele unaweka sahihi yako.

huu ni ubaguzi wa wazi wazi kwaserikali kutumia kodi za wananchi na kunufaisha vijana waccm pekee huku wale waliyo wa vyama vingine na ambao hawana vyama wakiishia kuona kodi zikiliwa na wachache, Naomba waziri kivuli aweze kufuatilia jambo hili mapema maana semina inaisha kesho. Nimeenda kwenye ofisi za chadema nikakuta wamewahi kufunga ofosi leo nikajua nikwavile ni ijumaa.
 
Hii serikali inanuka rushwa kila sekta, yaani kondi zetu wanapelekewa hawa wahuni wakazitafune?? CCM kwani hampati ruzuku??? Au ruzuku yenu ni kwenda kuhonga na hambakizi akiba ya kesho.
 
Yaani haya ma-escrow kazi yao wizi tu. Yaani mtu unasaini kwenye dashdash halafu wao wataenda kujaza sh 50,000! Kwa hiyo wanaiba sh 45,000 kwa kila mwanasemina.Ukoo wa panya huu!!!!
 
Yaani haya ma-escrow kazi yao wizi tu. Yaani mtu unasaini kwenye dashdash halafu wao wataenda kujaza sh 50,000! Kwa hiyo wanaiba sh 45,000 kwa kila mwanasemina.Ukoo wa panya huu!!!!

Hawa jamaa wamekuwa waathirika wa rushwa hawawezi kuacha hata kwa Dawa, sikio la kufa halisikii dawa.

CCM mmechokwa na Taifa hili kaeni pembeni nyie wezi wa nchi.
 
Hawo ni wezi wakubwa hawawezi kuficha aibu yao, yaani wanafanya semina za ccm kwa fedha zetu za umma???
 
Hiyo serikali imekwisha achiwa laana tokea wawamwagie wazee wa East Afrika maji wakawavulia nguo imekuwa laana kubwa sana kwao.
 
Napita nikirudi nipate jibu la kuridhisha kwa mamlaka iliyoidhinisha uchafu huwo.
 
hivi mwanga iko mkoa gani?

Ipo mkoani Kilimanjaro, Kunamtu mmoja hapa Anajiita pro Ikongo huyu mtu ameanza ulaghai wa kulaghai watu juu ya Ardhi alienda kwenye kijiji kimoja cha Lwami akamtumia mwenyekiti aliyemaliza muda wake na kumpatia fedha ili akawahonge wazee wa Lwami wampatie eneo la kijiji, yule mwenyekiti akala zile fedha akawapelekea wale wazee shilingi elfu 5000 mzee mmoja mwenye busara akasanua dili.

gia yao ilikuwa eti kuweka kitegauchumi cha vijana wa ccm hivyo wanaomba kijiji kiwapatie eneo hilo, kwasasa wanakijiji wameapata watalinda eneo hili bila hofu, sasa leo hii eti huyu prof ndiye anayeinjinia hayo mafunzo ya kihuni wanaoita ya vijana kumbe ni vijana waccm
 
Hivi bado tu kuna watu wanaambatana na ccm hadi leo??? Tena vijana???!!!!!!!!!!!.............
 
Back
Top Bottom