Wizara ya Maliasili na Utalii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Maliasili na Utalii

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nakuona, May 11, 2012.

 1. n

  nakuona Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kageshike na Nyalandu wanayo kazi kubwa sana ya kufanya katika wizara hii. Wizara hii inachangamoto nyingi sana
  ambazo tunaweza kama kuelezea kuja vitabu na vitabu. Lakini zifuatazo tutajaribu kuzielezea ili waone kazi waliyo nayo
  mbele yao.

  Wazawa wananyanyaswa sana katika sekta ya utalii, maeneo muhimu ya uwekezaji kama ya kujenga lodges na luxury camps wanapewa wazungu.

  Vitalu vya uwindaji wanapewa wazungu na wazawa wachache ambao wametoa rushwa.

  Leseni za uendeshaji kampuni za uwakala ni ghali sana kwa wazawa tofauti na nchi za jirani na sehemu nyingine. Kampuni ya uwakala wa utalii inalipa dola za kimarekani 2000 kila mwaka kama Tala(leseni) bila kujali kama wamepata wageni au wamekosa. Hii inasababisha kunyima fursa za kibiashara wazawa. Kwanini isiwe dola 300-500 kwa kampuni za watanzania na dola 5000-10000 kwa kampuni za wageni?

  Baadhi ya watendaji wakuu kwenye hii wizara wanamiliki kampuni zao za Utalii. Je wataweza kutenda haki kweli kama nao wanamiliki kampuni zao? Hili ni jambo ambalo Nyalandu na Kagesheki wanatakiwa waliangalie sana.

  Gharama za kwenda kwenye maonyesho ya utalii ni ghali sana chini ya TTB, jambo linalozuia wazawa kutafuta masoko
  sehemu mbalimbali.

  Viwangu vya kutua ndege katika viwanja vyetu vya ndege ni vya juu sana ukilinganishwa na nchi jirani...sasa madege makubwa yanashindwa kutua kwa wingi kutokana na hizi gharama. Pawe na mkakati yakinifu wakuweka mazingira ya kupendeza yatakayoruhusu madege makubwa kutua kwa wingi hapa Tanzania.

  Wadau kazi tu na moyo wa usikivu ndio utakaookoa wizara hii.
   
 2. S

  SokoroDar Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi Nyalandu si ana kampuni yake ya tours ? hakutakuwa na conflict of interest kweli ? au wanamiliki pamoja na mkulu ?
   
Loading...