Wizara ya maji na idara zake, nini kazi zao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya maji na idara zake, nini kazi zao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ziroseventytwo, May 27, 2012.

 1. Ziroseventytwo

  Ziroseventytwo JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 3,520
  Likes Received: 1,515
  Trophy Points: 280
  Salam Jf! Kwa ukweli mnaweza kunishangaa nitakapokiri hapa kuwa sijui kazi wanazofanya watu/watumishi walioajiriwa na wizara/idara ya maji. Hivi kazi zao nini? Kwa mfano Dsm pale makao makuu wizarani na kwenye vitengo idarani nini shughuli zao ikiwa Dawasco ndo wanashughulika na usambazaji na upatikanaji wa maji kwa wakazi wa jiji? Ikumbukwe dawasco ni kampuni,inayojiendesha kibiasha na inawafanyakazi wake. Ukija mikoani, kama k'jaro, idara ya maji wapo. Hawafanyi chochote,pale kuna kampuni ya JW ndo inayosambaza maji kwa wakazi wa mji wa moshi na vitongoji vyake,nayo kama Dawasco,ni kampuni inayojiendesha kibiashara na inawafanyakazi wake! Hivi hawa watumishi wa idara ya maji kazi zao ni nini? Inakuwaje watu wanapoamua kutumia nguvu na umoja wao kufuata maji toka milimani na kuyaleta kwenye vijiji kwa ajili ya mtumizi, then waje watu wa idara ya maji kuja kudai pesa, (kama bill ya maji) wakati maji yenyewe yalikuwa yanatiririka na kuingia mtoni na kwenda kusikojulikana.? Hivi wizara ya maji inahusika na maji yapi? Mto,bahari,maziwa, au na yaliyo chini ya ardhi? Mbona haya ya chini ya ardhi watu wanajichimbia na kuyatumia bila kuyalipia? Wao idara ya maji kazi yao ni nini? Kwani sifa ya kuajiriwa idara ya maji c kuwa tu plumber! Waje uraiani, mbona wapo wengi tu na manaendesha maisha fresh tu! Kwanini wizara ya maji isifutwe tukawa na mikataba kati ya halmashauri/manispaa/ au hata majiji na makampuni kwa ajili ya kusambaza maji kwa wakazi wa maeneo husika? Na wale wavijijini wakapata maji kupitia makampuni yanayochimba visima, na wakalipwa na halmashauri,. kupitia mikataba kati ya baraza la madiwani na makampuni ya uchimbaji visima, pale itakaponekana pana ugumu serekali kuu iombwe iongeze nguvu...kwa mtindo huu wa kuitegemea wizara/idara ya maji hatutafika. Nawasilisha!
   
Loading...