Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yalipa mishahara na matumizi mengine 1.7Bn isiyo na tija

ngararumu

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
468
188
Matumizi ya Bajeti ya Maendeleo
"Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa 2016/2017, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ilitengewa jumla ya Shilingi 100,527,497,000 kupitia Fungu 43 kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo. Aidha, Wizara ilipokea fedha kwa ajili ya kulipia madeniya wakandarasi wa skimu za umwagiliaji na kufanya fedha zilizoidhinishwa kuongezeka hadi kufikia Shilingi 101,527,497,000. Hivyo kati ya fedha hizo Shilingi 23,000,000,000 ni fedha za ndani na Shilingi 78,527,497,000 ni fedha za nje. Hadi kufikia tarenohe 20 machi, 2017 Shilingi 2,251,881,250 zimetolewa sawa na asilimia 2.22 ya Fedha zilizoidhinishwa. Matumizi ni Shilingi 1,731,271,924 sawa na asilimia 76.88 ya Fedha zilizotolewa. Kati ya Fedha hizo Shilingi 1,382,191,924 ni Fedha za ndani na Shilingi 349,081,000 Fedha za nje" alisema Waziri

Kwa hiyo basi,
Mwaka mzima wafanyakazi waliotakiwa kuisimamia miradi ya maendeleo walilipwa mishahara na matumizi mengine ambayo hayakuwa na tija kwa sababu fedha za maendeleo hazikupelekwa, kupata maendeleo kwa njia nin vigumu sana kwani tunashindwa hata ku utilize hata human resource tulioingia nao mkataba, je kuna ajira mpya hapo ambapo hiyo miradi ingestawi ingezalisha ajira
 

Attachments

  • upload_2017-3-30_13-42-16.png
    upload_2017-3-30_13-42-16.png
    73.9 KB · Views: 67
Ina maana kati ya Bilioni 101 zilizopitishwa kwa ajili ya matumizi kwa mwaka 2016/17, ni 2.2 bilioni pekee zilizotolewa (kupelekwa wizarani)? au mimi sielewi? kama ndio hivyo ninavyofikiri kuna hatari ya kuwa na bajeti hewa kwa mwaka 2017/18.

Pia nakubaliana na hoja yako ya kuwa na wataalamu ambao wanalipwa bila kutekeleza wajibu wao.

"Lete Vyeti"
 
Hii ni hali ya kawaida kwa watumishi wa Idara zote. Kufika kazini maana yake ni kusaini asubuhi saa moja na nusu. Na kufanya kazi maana yake ni kupiga stori ofisini hapo, majungu na siasa hadi saa kumi kasoro na kisha kurudi nyumbani. Kila siku hali ndio hii ila mwisho wa mwezi mshahara kama kawaida.
 
Back
Top Bottom