illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Poleni na majukumu mazito ya serikali hii ya viwanda, kuna changamoto nyingi sana kwa waajiri ambazo sijawahi kusikia zikizungumziwa kiukweli zimekaa kimaslahi zaidi, ndugu zetu wanao fanya kazi kwenye makampuni ya ulinzi na mahoteli nadhani ni wahanga wakubwa wa hili inasikitisha kuoma mwajiri anakulazimisha uweke pesa zako benki fulani bila shaka hapo ananufaika inasikitisha zaidi pale ambapo mwajiri anakulazimisha uchangie mfuko wa jamii fulani kitu amnacho ni kinyume na haki za mfanya kazi, tuje kwa ndugu zetu madereva wa malori na mabasi, nchi yetu inatumia usafiri wa ardhi kwa asilimia zaidi ya themanini kusafirisha mizigo na abiria inasikitisha sana kama wakazi wa jiji kama Dar wanategemea vyakula kutoka mikoani ambavyo vinakuja na barabara pia tunasafirisha mizigo mingi inayokuja na bandari kwenda nchi jirani kwa kutumia barabara lakini asilimia zaidi ya sitini na tano wa makampuni haya ya usafirishaji hawana ajira rasmi badala yake kuna. VYama ya madereva ambavyo mara kadha vimegeuka kuwa vya kisiasa au kutumika vibaya tunaona jinsi maderva wanapopata maradhi au ajali wanavyokuwa hawatambuliki na wamiliki wao kero zipo nyingi ila tuanze na hayo kwanza manake ni kama watunwengi hawajui majukumu ya wizara hii.