Wizara ya Elimu yakanusha kuzuia wenye Diploma kwenda chuo kikuu

Serikali ya wakurupukaji hii. Wakitoa matamko yao ya kukurupuka wanasubiri kuangalia reaction, reaction ikiwa ni very negative wanabadili kauli, "Nilinukuliwa vibaya"
Waziri alikuwa very clear ktk Maelezo yake.

Issue hapo ni mleta mada ndani ya JF ndiyo aliitoa vibaya.

Hii tabia sasa hivi unaanza kushamiri na ndiyo maana Rais mstaafu Mwinyi alipoenda kumuona Rais Magufuli Ikulu aliliongelea hili kuwa watu wanapotosha sana Hotuba za Rais Magufuli kwa malengo yao.
 
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Amedai kuwa Serikali haikukataza na Kwamba Waziri alinukuliwa vibaya.

Full kujichanganya kwa matamko kama mnara wa Baberi
Chanzo: Clouds FM
Waziri ametoa Maelezo very clear shida ni kuelewa alichosema kwa baadhi ya watu yenye mitazamo hasi dhidi ya Serikali ndiyo shida.

Na huu mpango wa kupindisha Hotuba za Serikali kila kukicha kwa kisingizio cha uelewa nadhani kuna haja ya kutafutiwa dawa yake.

Linaweza kutokea jambo kubwa hapa nchini na watu wakajua ndiyo uzushi tu kumbe issue ni serious.
 
Sasaivi uprofessor Tz si elimu ya juu tena mtu kujitambua kwa taalauma yake, mtu anaweza kuropoka lolote muda wowote, elimu Tz sasa imekuwa kama ndoto. watu wanaongozwa ni matamko tu alimradi wawe wamepiga marufuku kitu chochote wanapokuwa kwenye majukwaa wakionekana kwenye tv.
 
Waziri alikuwa very clear ktk Maelezo yake.

Issue hapo ni mleta mada ndani ya JF ndiyo aliitoa vibaya.

Hii tabia sasa hivi unaanza kushamiri na ndiyo maana Rais mstaafu Mwinyi alipoenda kumuona Rais Magufuli Ikulu aliliongelea hili kuwa watu wanapotosha sana Hotuba za Rais Magufuli kwa malengo yao.

Wewe ulimsikia wapi Mwinyi akimuambia Magufuli hivyo? walizama ndani wakiwa 2 peke yao tu zaidi ya saa 4 wanaongea, basi tueleze na hayo mengine walioongea.
 
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma diploma katika mambo kama uganga (clinical medicine), ufundi (technical education), kilimo (agriculture) etc. Lakini sharti wawe wamefaulu kidato cha 4na kuchaguliwa kusoma vyuo vya kati.

Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma, na diploma zao hazitaruhusiwa kutumika kama equivalent pass ya kujiunga chuo kukuu hadi watakaporeseat. Diploma watakaoruhusiwa kusoma degree ni waliopita form six, au waliofika form four wakafaulu na kuchaguliwa kwenda vyuo vya kati.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.
 
Walioikomalia walikuwa ni ma-ccm! Hukuwaona akina jingalao, stroke na Lizaboni?
Huyu jamaa ni kama roboti. Hajua kama waliokuwa wakisifia uamuzi huo ni Lumumba wenzake. Yeye ameshakuwa programmed kuwa lazima neno moja au yote kati ya haya " Bavicha, Mbowe na Chadema" yatokee kwenye thread zake. Pitia zote utaona.
 
Wewe ulimsikia wapi Mwinyi akimuambia Magufuli hivyo? walizama ndani wakiwa 2 peke yao tu zaidi ya saa 4 wanaongea, basi tueleze na hayo mengine walioongea.
You need a clip umsikie mwenyewe.
 
Wazingatie alichoshauri Mzee Mkapa, rais mstaafu wa awamu ya 3 na waziri wa zamani wa wizara ya elimu ya juu.

Tusitake kuchezea mfumo wa elimu. Ni hatari. Dunia kote kuna alternative entrance qualifications ya kujiunga na mafunzo ya kozi mbalimbali za shahada za vyuo vikuu. Sifa hizi huwekwa na vyuo vikuu husika kwa kozi husika. Haziwekwi na wizara ya elimu. Hata hizo foundation courses huwekwa na vyuo husika kuwawezesha wahusika kumudu masomo husika ya shahada hizo na wizara ya elimu haina uhalali wa kuingilia.

Wizara ya elimu au serikali ni kuhakikisha kuwa final products (wahitimu wa vyuo vikuu) wana ubora wa kiwango kinachokubalika. Wizara lazima iwe na mechanism ya kupima final products hizi na kuweka masharti ya kua accridate vyuo vikuu. Si kazi ya wizara kuingilia mchakato (process) ya utengenezaji wa hizi products. Serikali ikishajiridhisha kuwa chuo husika kimekidhi masharti ya kuwa chuo kikuu na kukipa acreditation basi kiwe huru ku process watalaam hayo na serikali iwe na mechanism ya kupima ubora wa wahitimu hao huko makazini walikoajiriwa.

Hivi kweli Wizara ina ushahidi gani kwamba ubora wa wahitimu wa shahada hizi ni hafifu kwa wale waliojiunga na vyuo hivi kwa sifa za alternative qualification eg ordinary diploma, foundation course etc? Kuna ushahidi gani kwamba PhD aliyopata mhitimu aliyejiunga chuo kikuu kwa shahada yake ya kwanza kwa alternative qualification ni hafifu ukilinganisha na yule aliyejiunga kwa direct qualification ( Division 1 form 6)? Yaani PhD kwa mfano ya Ndalichako (direct) ni bora zaidi ya Dr X (indirect)? Jamani tuwe realistic. Hapo kwenye ma Dr X nasikia wamo mawanasheria mahiri kama Dr Mwakyembe, mwalimu wa Tundu Lissu alipokuwa chuo kikuu. Mwakyembe tunaambiwa kuwa baada ya form 6 alijiunga na kozi ya diploma ya uandishi wa habari, diploma hiyo ndiyo ilimuwezesha kujiunga shahada ya sheria UDSM kwa alternative entrance qualification. Wapo wengi tu na ni mahodari kweli kweli kwenye taaluma zao.

Tuliopataga Division one form six tusijione kwamba ndiyo wenye akili kuliko wengine na kuwa hao wengine hawapaswi kupata hayo madigrii milele na hawana fursa ya kujiendeleza kwa njia yo yote nyingine isipokuwa kurudia masomo yote ya form 6 eg PCB! Hivi ni kiasi gani ya material ya PCB yanatumika kusoma shahada ya uganga? Ni kiasi gani cha masomo ya diploma ya miaka 3 ya clinical medicine inatumika kusomea masomo ya shahada ya uganga? The answer is obvious, the responsible universities know it. The final quality of the products are known to everybody and anybody who wants to research on the two final products is welcome. No research no talk. This is is the advice to Ministry of Ndalichako.
 
Elimu ya form six ni ya kizamani bora ifutwe tu ukimaliza form four unaenda VETA kwanza kujifunza ujasiriamali then Chuo Kikuu.
Wewe na waziri ndalichako hamna tofauti, weka case studies zinazothibitisha hiyo kauli yako.
 
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi wasio na sifa kujiunga kujiunga na masomo ya Shahada (degree) kwa kupitia Foundation Course (kwa wasiofaulu kidato cha sita).

Prof. Ndalichako amesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.
sifa ni zipi....swali kwamba vyuo vya nje Ikiwa EE mbili napata vyuo vyenu vya kiha vina lipi cha ajabu
 
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imetoa ufafanuzi kwamba haijapiga marufuku watu wenye Stashahada wenye sifa kujiunga na vyuo vikuu badala yake walichokataza ni wanafunzi waliofeli kidato cha nne na cha sita kujiunga na vyuo vikuu bila kuwa na vyeti vyenye sifa.

Aidha, imesema kwa waliomaliza kupitia mfumo huo na wapo kazini ni wajibu wa waajiri wao kuhakikisha wana sifa za kazi wanazofanya na kutumia fursa hiyo kufanya mitihani ili kuwa na sifa zinazohitajika.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya alitoa ufafanuzi huo jana Dar es Salaam kutokana na taarifa za upotoshaji zilizoenea mitandaoni kwamba serikali imepiga marufuku watu wenye Stashahada kujiunga na vyuo vikuu badala yake watakaoingia ni wenye sifa za kidato cha sita.

Manyanya alisema kwa waliopo vyuoni kwa sasa wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa na sifa za shahada kwa kusafisha vyeti vyao na wapewe fursa ya kufanya mitihani hiyo waliyofeli na kama wamefaulu kozi hiyo, pia wataweza kufaulu mitihani hiyo itakayowapa sifa ya kusoma vyuo vikuu.

“Ni vitu tunavyovifanya wenyewe ila vina madhara makubwa, unakuta mtu anakaa nafasi kwa sababu ana vyeti, lakini uwezo hana… uhakiki utafanyika kwa vyeti na wanaofanya hivyo ni Utumishi,” alisema Naibu Waziri.

Alisema kwa watakaobainika pia kuingia vyuoni kwa sifa ambazo zilikuwa hazitakiwi kwa wakati huo ni batili zitafutwa na kwa watakaoingia kwa sasa vyuoni kwa kutumia njia zisizo rasmi na kubainika hata ikifika mwaka 2020 watafutwa kwa kuwa taarifa tayari wanayo.

“Kilichoongelewa siku ile ni kuruhusu kidato cha nne na kidato cha sita waliofeli kuingia kwenye ‘foundation course’ na diploma haikutajwa pale kwa kuwa haikuulizwa na hakuna kauli iliyotajwa pale kukataza watu wa diploma kwenda chuo kikuu,” alieleza Manyanya akirejea kauli ya Waziri wake, Profesa Joyce Ndalichako hivi karibuni katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) yaliyofanyika mkoani Pwani.

Profesa Ndalichako alikaririwa akisema vigezo vya udahili vinatakiwa kuzingatiwa.

“Nami ningependa nizungumzie kwamba foundation course hazimuongezei mtu sifa. Kama sifa ya kujiunga na chuo kikuu ni kufaulu kidato cha sita, kama amefeli Baraza la Mitihani linaruhusu kurudia mtihani, kwa nini anakwepa kule? Kwa nini? Kwa nini tunataka tuendeleze uchochoro,” alieleza Waziri Ndalichako.

Naibu Waziri alisema kuna njia mbili za kwenda chuo kikuu ikiwemo njia ya moja kwa moja na njia ya mbadala ya kuwa na vyeti vinavyotambulika na kinasimamiwa na mamlaka husika ambayo ni Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na wawe na ufaulu mzuri.

“Tanzania imejiwekea mifumo yake ya elimu ambayo inaendana na ngazi za kimataifa katika utoaji wa elimu na hapo awali tulikusudia kuhakikisha elimu inatolewa kwa watu wengi zaidi na hizo fursa zinawafikia wadau wote katika ngazi mbalimbali kwa kupanua elimu ya msingi hadi vyuo vikuu,” alieleza Naibu Waziri.

Alisema walitambua kuna wadau mbalimbali walitamani kusoma vyuo vikuu, lakini hawapati hiyo fursa na ndiyo wakaanzisha mfumo huo wa Chuo Kikuu Huria na mtu anaweza kusoma alipo na mfumo umekuwa ukiboreshwa siku hadi siku.

Alisema iliwekwa mifumo ya vyeti na ngazi zake kulingana na vigezo na hivyo siyo kila cheti kinachotolewa kinaruhusu mtu kwenda ngazi nyingine na kila mamlaka imepewa jukumu ili kulinda ubora wa elimu unaotolewa nchini.

Naibu Waziri alisema kutokana na uanzishwaji wa vyuo mbalimbali kumejitokeza changamoto na watu kutoka katika mfumo rasmi uliopangwa na kujiwekea mifumo binafsi ambayo imeingiza hata wanafunzi wa kidato cha nne ambao hawana sifa kuingia vyuo vikuu.

“Jambo hilo limesababisha kuwepo kwa msuguano, haiwezekani mtu afeli kidato cha nne bila kuwa na cheti kingine chochote anaingizwa katika kozi hiyo halafu anaingizwa chuo kikuu, sisi hatujarasimisha mfumo huo wa ‘foundation course’ na hatuna vipimo vyake,” alieleza.

Alisema kwa kawaida mwanafunzi mwenye diploma inayotambulika wamewekewa usawa wa alama fulani na kidato cha sita hivyo wanakuwa na sifa ya kuingia vyuo, lakini siyo waliofeli hivyo wanatakiwa kufanya utafiti zaidi katika kozi hiyo.

“Haiwezekani kila mtu akajianzishia mfumo wake tu, tulifikia eneo ambalo si zuri kama nchi na sasa tutaimarisha ubora…ukifeli kidato cha nne unatakiwa kwenda kusoma na kupata cheti kwenye mtaala unaotambulika na ukaenda diploma na unapofaulu unaweza kwenda chuo kikuu,” aliongeza.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila alisema suala la ‘Foundation course’ limelenga kumuandaa mtu mwenye sifa ambaye amekuwa nje ya mfumo kwa muda mrefu ili kuingia chuo kikuu, lakini walichokuwa wakikifanya wengi ni kuwachukua waliofeli kidato cha nne na sita na kuwaingiza katika kozi hiyo na hatimaye kuwaingiza chuo kikuu.

Awali, baadhi ya wadau wa elimu nchini waliozungumza na gazeti hili wakiwemo wanataaluma walisema wanasubiri kupata taarifa rasmi kutoka wizarani kuhusu madai hayo, lakini wakaeleza manufaa ama athari za kutumika kwa mfumo huo nchini.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dares Salaam, Dk Benson Bana alisema haamini iliyonukuliwa ilikuwa kauli rasmi ya serikali, lakini akaongeza, “Upo utaratibu mbalimbali wa kuingia vyuoni na walio wengi wamepitia mfumo wa kuanzia cheti na kujiendeleza hadi kufika chuo kikuu na kutunukiwa digrii wakiwemo maprofesa na madaktari wengi.”

Alisema mfumo huo unasaidia kupata wanafunzi wengi wenye uzoefu na ambao huwasaidia wenzao katika kufanikisha elimu yao na huo ndio mfumo unaotakiwa

Dk Bana alisema jambo linalotakiwa kutazamwa ni uwepo wa vyuo vingi vikuu ambavyo vimekuwa vikigawa alama za ajabu kwa wanafunzi, lakini wanapoingia vyuo mtihani ndio utakaowapembua.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch alisema “Elimu ya kujiendeleza kuanzia ngazi ya cheti na kuendelea diploma, digrii na hata kufikia uzamivu ni mfumo uliopo dunia nzima.”

Alisema wapo wataalamu mbalimbali nchini na hata maprofesa ambao hawakusoma katika mfumo huo wakiwamo walimu wake (Ndalichako) waliosoma kupitia mfumo huo.

Imeandikwa na Hellen Mlacky, Lucy Lyatuu na Regina Kumba-Habarileo.
 
Kumbe ni kweli hajatamko hilo bwana, ndo nimesikiliza hiyo clip, hajatamka lolote kuhusu hilo swala.

pole mama Ndalichako kwa kulishwa maneno ya Uongo na utapeli na Nyumbu.
 
Alisema mfumo huo unasaidia kupata wanafunzi wengi wenye uzoefu na ambao huwasaidia wenzao katika kufanikisha elimu yao na huo ndio mfumo unaotakiwa.

Dk Bana alisema jambo linalotakiwa kutazamwa ni uwepo wa vyuo vingi vikuu ambavyo vimekuwa vikigawa alama za ajabu kwa wanafunzi, lakini wanapoingia vyuo mtihani ndio utakaowapembua.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch alisema “Elimu ya kujiendeleza kuanzia ngazi ya cheti na kuendelea diploma, digrii na hata kufikia uzamivu ni mfumo uliopo dunia nzima.”

Alisema wapo wataalamu mbalimbali nchini na hata maprofesa ambao hawakusoma katika mfumo huo wakiwamo walimu wake (Ndalichako) waliosoma kupitia mfumo huo.

Imeandikwa na Hellen Mlacky, Lucy Lyatuu na Regina Kumba-Habarileo.
uwe unaangalia previous post
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom