ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Hatujasikia tamko lolote toka kwa wahusika juu ya ukosefu wa vitabu vya kufundishia kwa wanafunzi wa darasa la tatu nchi nzima.
Ikumbukwa kwamba hawa wanafunzi wa darasa la tatu wanatumia mtaala ambao kimsingi unatofautiana na wanafunzi wengine , wao ndio waanzilishi wa mtaala mpya ambao kwa mtaala wao watatakiwa kumaliza elimu ya msingi wakiwa darasa la sita na sio la saba kama ulivyo sasa. Wao mtaala wao unawataka kusoma masomo sita tu tofauti na wenzao wa madarasa ya nne, tano, sita na saba ambao wanasoma masomo kumi. Na wao darasa la tatu kwa mujibu wa mtaala wao ratiba ya vipindi vyao hutakiwa kuisha saa sita na nusu mchana baadala ya saa tisa na dakika ishirini jioni.
Mpaka leo nchi nzima serikali haijapeleka vitabu vya masomo mawili yaani somo la maarifa ya jamii na somo la uraia na maadili , hivyo kuwafanya wanafunzi hao kusoma masomo manne tu tangu shule zimefunguliwa kwa sababu walimu hawajui wafundishe nini na mada zipi.
Kama wahusika wameshindwa kuendesha mtaala huu mpya ni vema waziri mwenye dhamana atoe waraka wa kuwataka walimu wafuate utaratibu wa kuwafundusha wanafunzi hao. Kwa sababu nimetembelea shule mbalimbali nimekuta baadhi ya walimu wakifundisha somo la kiingereza wengine wakitumia vitabu vya darasa la tatu na wengine wakitumia vitabu vya darasa la pili na wengine wakitumia vya darasa la kwanza kwa sababu serikali haijaleta vitabu vyake na ukizingatia kwa mtaala wao somo la kiingereza wanaanza kusoma wakiwa darasa la tatu, sasa swali la kujiuliza mtoto ambaye hajasoma somo la kiingereza darasa la kwanza, darasa la pili hajajifunza hata misingi yake halafu darasa la tatu mwalimu amfundishe kwa kutumia kitabu cha darasa la tatu ataelewa nini.
Kwa kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yoyote dunia nilitrgemea wasomi, wanasiasa na waandishi wa habari wangehoji hilo kwa ajiri mustakabali wa dira ya elimu yetu.