Wizara ya Elimu inanishangaza!

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi imetangaza mafunzo ya vijana waliohitimu kidato cha sita kujiunga na masomo ya awali (Pre-entry) kwa ajili ya kuwaandaa kusomea stashahada ya ualimu. Mafunzo hayo yatachukua miezi mitatu na yatafanyika katika vyuo vichache vya ualimu katika kanda. Jambo la kushangaza ni kwamba vijana watakaojiunga na mafunzo hayo wanapaswa wawe na sifa za kujiunga na stashahada. Sasa kama wanazo sifa, hayo mafunzo ni ya nini tena?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom