Wizara ya Elimu imelala; fedha za walipa kodi vyuo vya ualimu zimekuwa mtaji wa wakuku wa vyuo!

Oltung'anyi

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
284
196
Ndugu wadau, mimi kama mdau wa elimu na ninayesomesha nimesikitishwa sana na malalamiko kutoka vyuo vya ualimu nchini. Malalamiko haya yanakuja kipindi ambacho waalimu katika vyuo hivi wakiwa katika zoezi la kufanya assessment kwa waalimu wanafunzi walio katika shule mbalimbali za msingi na sekondari kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu ya kufundisha kwa vitendo.

Wakufunzi wamelalamikia matumizi mabaya ya fedha zinazotumwa kwa ajili yao ili kufanikisha zoezi hili la assessment. Inasemekana kuwa wakuu wa vyuo wamefanya taarifa za fedha hizi kuwa siri, hali inayotafsiriwa kuwa ni mbinu yao ya kujineemesha na mafungu haya kwa kuwa wakufunzi wamenyimwa fursa ya kufahamu uhalisia wa mafungu haya ya fedha. Baadhi ya vyuo vilivyo na Utata wa matumizi ya mafungu haya ya fedha kwa ajili ya posho ya wakufunzi kwa ajili kufanya assessment wakati wa zoezi la Block Teaching Practice (B.T.P) ni kama chuo cha ualimu cha Mtwara,chuo cha Ualimu Kinampanda -Singida, chuo cha ualimu Dakawa-Morogoro, Mhonda-Morogoro. Hivi ni baadhi, kiujumla hali inaonesha kuwa vyuo vingi vimekuwa na mijadala mirefu kuhusiana matumizi ya fedha hizi za wizara kwani imeonekana dhahiri wakuu wengi wa vyuo kufanya fedha hizi za walipa kodi kuwa ni mitaji yao.
Ndugu wadau, hali hii inasikitisha. Walimu wanaowaandaa walimu wanakandamizwa, wanaonewa na kunyanyaswa. Mimi kama mdau wa elimu, hali hii inakera na sio ya kuvumilia. Nimeona niwashirikishe kama nami milivyoshirikishwa jambo hili ili kwa pamoja tuone tunawasaidia vipi wanyonge hawa. Serikali kupitia wizara yake ya Elimu na mafunzo ya ufundi, iliangalie jambo hili kwa undani na ichukue hatua!

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom