Wizara ya ardhi tutengenezeeni michoro kama hii kwa miji yote kwa pamoja

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Yupo mkereketwa mmoja kwenye jamii forum ameweka ramani hizi akilinganisha Dar na Nairobi, lakini kwa nini tusiwaulize wizara ya ardhi watueleze ramani kama hizi kwa miji yetu yote iko wapi?

386858-0939a25c21df571ef059f4d574557ae0.jpg

386859-07656273e95cb0acb383740ee2c0cb96.jpg




serikali kuu ikishakuwa na hii mipango basi wanatekeleza kulingana na mji ulivyopangwa, halmashauri zinatekeleza majukumu yao katika ramani hizi kupelekea miji yetu ifanane hivyo.

watu binafsi wanaaanza kuendeleza kuelekea miji kufanana hivi.

tukijipa miaka kadhaa ya kubadili miji yetu kuelekea kwenye mipango iliyoko chini kila mdau akiiona nina uhakika tutafika

lakini kwa sasa mwananchi anaweza kusimamisha ghorofa leo kesho anabomolewa maana hakuna anayejua mipango ikoje kwa kila sehemu. Sio serikali sio watu binafsi hakuna anaejua bali wakipisha mradi mmoja ndio wanatanguliza sheria inasema hivi.

ni jukumu la serikali kutumia sheria mbalilmbali kuweka mipango chini ndio tutafika na kila mmoja ajikite katika kutimiza ajibu wake katika hilo.
 

Attachments

  • 1.png
    1.png
    163.2 KB · Views: 61
  • 2.png
    2.png
    82.8 KB · Views: 36
Wewe unategemea watu kama akina bashite waliopata digrii kwa kuwatumia watu wa karibu nao wanaweza kutengeneza kitu kama hicho?
 
Back
Top Bottom