Wizara ya Ardhi: Tumbueni majipu katika jiji la Mwanza

treborx

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
4,621
2,223
Wadau,
Nimekuwa nikihangaika kubadilisha umiliki wa kiwanja nilichokinunua huko Mwanza tangu Mwaka 2014. Nataka kufuata taratibu halali ili nilipe kodi za serikali na sitaki kabisa kutoa rushwa. Lakini tangu mwaka 2013 nimekumbana na urasimu wa kutisha mpaka naanza kuhisi kama vile nitakuja kukipoteza kiwanja hicho. Jiulize umenunua kiwanja kwa mtu (Kiwanja kina ofa tu) tangu mwaka 2013, na tangu wakati huo kiwanja bado kina jina la mtu aliyekuuzia. Akiamua kukiuza kwa mtu mwingine utafanyaje?

Mdau mwenye kujua wahusika wakuu wa masuala haya huko Mwanza, naomba msaada wake. Ardhi Mwanza wanatisha kwa urasimu. Mzee Lukuvi kama anatafuta kesi za ardhi Mwanza niko tayari kumpa hii pia.
 
Mkuu suala la kubadilisha umiliki liko mkononi mwa mnunuzi na muuzaji kwa maana ya kukamikisha documents zinazohitajika. Unatakiwa kuwa na sale agreements, valuation report ya kiwanja iliyoidhinishwa na mthamini wa serikali, fomu za kuonyesha kusudio la kuhamisha miliki (huandaliwa na mwanasheria), ulipe capital gain (TRA) na concert. Kama umekamilisha vitu vyote hivyo na bado unazungushwa una haki ya kuandika complaint kwa Mkurugenzi wa Jiji.
 
Back
Top Bottom