Wizara ya Afya nauliza swali..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Afya nauliza swali.....

Discussion in 'JF Doctor' started by Mess, Aug 21, 2012.

 1. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini kuna watu wanasema wanatoa sumu mwilini, kuna watu wanasema wana vipimo vya magonjwa 29, kuna watu wanasema wanatibu vidonda vya tumbo, kansa, sukari, HIV n.k.

  Hawa watu hawajajificha na wengine sasa hivi wanajiita ma professor eti kwa kudanganya watu na wamefungua vituo vyao, kama huyu askofu Gamanywa n.k. Tuelezeni watanzania kama wanachosema ni kweli otherwise muwa-stop, hawa watu wanatajirikia kwenye migongo yetu sisi maskini ambao tumeshidwa kupata majibu ya magonjwa yetu na wazazi wetu wanaoumwa.

  Binafsi inaniuma sana, maana unaenda hospital hizi unaona kabisa wanakudangaya ila kama umempeleka mzazi inabidi uvumilie tu maana ukionekana kukosa imani mgonjwa ndo umemuua kabisa.

  Kazi kwenu bwana.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Cancer haina tiba bado lakini dawa ya ukimwi ipo lakini haijahalalishwa...Na ninaweza kusema sidhani kama serikali nyingi hapa duniani zinataka dawa ya ukimwi zithibitishwe na kuanza kuuzwa madukani kwa sababu kila mtu akishajua dawa ipo hakuna atakaenunua condoms...na si mnajua condoms ni biashara kubwa sana hivyo viwanda vitafungwa..pili watu wakiwa hawatumii kondom mimba zitaongezeka watoto wataongezeka ambayo hiyo pia itakua mzigo mkubwa hasa kwa nchi za ulaya ambazo wanakupa allowance(fedha) za matumizi ya mtoto. So ukija kuangalia mwisho wa siku sidhani kama wako tayari dawa ya ukimwi ithibitishwe na ianze kuuzwa madukani.
   
 3. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  ni kweli niliwahi kusikia serikali ikitoa taarifa bungeni kwamba si sahihi na pia vyombo vya habari havitakiwi kuruhusu hayo matangazo lakini cha ajabu hao watu wameendelea kujitangaza magazetini bila kuchukuliwa hatua yoyote.Pamoja na kuamini kuwa baadhi ya dawa za kienyeji zinatibu vizuri lakini si sahihi kwa utaratibu wanaotumia kwani kuna watu matapeli wanaweza kutumia mwanya huo badala ya kuokoa maisha ya mtu tukawa tunazidisha madhara
   
 4. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  thanks, lakini nadhani swali langu la msingi hujajibu
   
 5. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  rodrick alexander, hili ni janga sana. Mimi baba yangu alikuwa anaumwa kila siku nampeleka hapo sinza kwa watu wanajiita wanatibu magonjwa sugu kila nikimpeleka wanasema anaendelea vizuri sasa wanampima tena elfu 62 natoa kwa muda wa miezi sita na appointment zao ni week 2 2, sasa hapo nikimwambia mzee kuwa jamaa tapeli nimemuua maana hana matumaini mengine yoyote.
   
 6. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa hapa Arusha ukiingia makumbusho ndani ana kiofisi anajiita professor, kipimo kimoja ambacho yeye anadai kinaona magonjwa zaidi ya 60 ni elfu 25. Harafu anatibu magonjwa yote, hata mimi sielewi na kwanini wananchi wasielemishwe kuhusu haya mambo na wizara? Babu wa Samunge, mpaka viongozi wetu wakuu waliingia huko. Sijui la kufanya wajanja acha wale pesa zetu masikini
   
 7. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Au na viongozi wetu hawajui kuwa hawajui majukumu yao, kama na wenyewe walitililika Samunge basi madaraka yao wanayachukulia kisiasa zaidi sio kiuhalisia. Inakuwaje daktari anachukua muda mrefu kumpima mgonjwa kuchukua stool, urine, blood na vitu vingine then Gamanywa atumie dakika 5 kupima system za mwili zote bila kutoa damu, choo, mkojo n.k na bado anatoa sumu zote mwilini???? mbiona hakumuita Mwakyembe amtoe sumu kama ana uwezo huo?? Binafsi naona ni wezi wanaofugwa na serikali hasa wizara ya afya. Vituo vya Gamanywa vinatangazwa sana redioni na wanatumia popoluarity waliyoipata kwenye dini kuibia watu. Mimi bado siamnini kuwa wanaweza kupima hivyo vipimo na kama wanaweza toa sumu mwilini.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swali lako usiwaulize wizara ya afya, liulize Bunge la jamhuri. Kama hakuna sheria inayowakataza watu kuuza au kutangaza tiba mbadala wizara ya afya itawafanya nini? Sheria zinatungwa na Bunge na kutafsiriwa na mahakama na kusimamiwa na utekelezaji na Polisi.
   
 9. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimewauliza wizara kwa sababu hivi majuzi walisema dawa za vidonda vya tumbo hazijathibitishwa na wizara kama yule mama anayetibu anavyojitangaza, lakini kukanusha kitu hiki hakukutumia efforts sana kama yule mama anavyotumia efforts kujitangaza. hivyo nikajua kumbe wizara ndiyo inayo certify vitu hivi. Hivyo nina uhakika sheria ipo, ila watu hawawajibiki tu
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Iwapo mganga atataka dawa iwe certified anaenda TFDA na ikikidhi viwango inakuwa registered. Lakini hiyo haitoshi, inatakiwa iwepo sheria ya kuwakataza watu kuuza dawa ya kienyeji kiholela, lakini hilo swala siyo rahisi sana kwa sababu mpaka kati ya dawa na chakula ni mwembamba sana.
   
 11. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  kile ni kichaka na si wizara ya afya
  mtaani kila mtu anajiita doctor, mfamasia, nesi, mtaalam wa maabara na kada nyingine za afya wakati watu hata hawakuwahi kuisoma fani hii, hawajui chochote, mathalani kuna mtu mmoja anajiita manywele anaongopea watu yeye ni GYNOCOLOGIST na ni PAEDIATRICIAN wakato s kweli na kuanza kuwapanga akina mama na watoto zao na kuwachuna hela zao na kibaya zaidi nyuma ya duka lake hili la dawa kuna kituo cha Polisi, sasa unategemea mambo kama haya nani wa kuyasimamia, kwa nini watanzania wasipate usugu wa dawa kwa kupewa dawa zisizohusika tena toka kwa watu wasioielewa fani hii ya dawa na magonjwa, cha ajabu yeye anakuwepo kuanzia jioni na kuwaongopea asb yuko muhimbili wakati hafanyi kazi hapa.
   
 12. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uhuni kule kwetu kuna dispensary zilifungia baada ya week zote zikafunguliwa tena kwa majina tofauti mmiliki yule yule ila jina limebadirika mpaka wengine wanatumia majina ya St. something
   
 13. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Basi wanaohusika saidieni wananchi wanapata shida, na matapeli wakineemeka
   
 14. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ebu ona sasa, hivi ni lini tutakuwa na uwajibikaji kazini. Watu wanajua kazi ni kukabidhiwa ofisi tu na kufanya kasherehe ka kifamilia basi. Nakumbuka jamaa wa vitambulisho vya taifa alipotangazwa kupewa ile nafasi alifanya sherehe kubwa sana akidhani kazi ndogo, lakini ingekuwa uwajibikaji umo sasa hivi angekuwa out.
   
Loading...