Wizara ya Afya na Chips za Dar!

Wizara ya Afya na Chips za Dar!

yusufummaka

Member
Joined
Apr 7, 2012
Posts
30
Reaction score
20
Kumeibuka biashara jijini DSM ya kila kona ya jiji kuwashwa moto na kukaanga chips mitaani. Wauza chips na mishikaki hawa hawafahamiki nani kawawapa kibali bila ya kufahamu kama afya zao na mazingira ya biashara vinakidhi haja ya kuwauzia wenzao vyakula. Biashara hii inawatia wananchi kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa kama: typhoid, cholera, minyoo, na kuhara damu. Pia, iko hatari ya mioto hii ya holela barabarani kuunguza waendao kwa miguu kandokando mwa barabara pamoja na kuunguza nyumba zilizo karibu na majiko hayo. Hivi wizara ya afya inasubiri mabaya yawapate wananchi ndiyo ichukuwe hatua?
 
Umesahau kugusia matumizi ya mafuta machafu na mafuta kuchanganywa na kemikali mbalimbali kama mafuta ya transfomer etc.
 
machinga walivyojengewa ule mjengo wa chinga complex walishindwa kivuli cha ndani wakaamua kurudi kwenye jua!ikiwa kina mama majumbani wanawasha majiko nje ya nyumba na kupika wakati ndani kuna jiko!!mitaani si ndio itakuwa utamaduni wetu!
USHAURI:
tulieni hiyo imeshakuwa tabia yetu ipo ndani ya mishipa yetu ya damu!
huwezi kugeuza tanzania kuwa ulaya!utakufa kwa presha bure!
 
hiyo mishkak yao huwa hata sijaribu kuisogelea. Niliwah kumsikia jamaa flan kwenye 'pawabreki fasti' {radio clous} akiongea na bonge jinsi anavyochinja paka na kuuza nyama kwa njia ya mshkak, nilitapika chai yangu ya maziwa. Hasa nikikumbuka wakat wanaanza anza mwaka 2001 nilikuwa nimepigika nilikuwa nahudhuria sana kwa hao jamaa. Na nyama yenyewe ilikuwa lainiii!!
 
Bora wawaache tu kwani pindi watakapoamua kuwaondo watakuwa wamewapa kula mgambo watakaokuwa wanawaondoa kwakuchukua rushwa na kuwaacha mfano ni machinga pale k.koo mgambo wamekuwa wakipita na kukusanya chao na pindi ukiona wamemkamata mtu ujue kagoma kutoa rushwa
 
Biashara ikishamiri ni ishara yakua kuna soko la biashara husika!
Wizara ya afya hata takwimu za vitanda vya kulazia wagonjwa hawana sembuse chips vumbi mtaani? Acha watanzania wajipatie kipato chakutunza familia zao.
 
Kumeibuka biashara
jijini DSM ya kila kona ya jiji kuwashwa moto na kukaanga chips mitaani.
Wauza chips na mishikaki hawa hawafahamiki nani kawawapa kibali bila ya
kufahamu kama afya zao na mazingira ya biashara vinakidhi haja ya
kuwauzia wenzao vyakula. Biashara hii inawatia wananchi kwenye hatari ya
kuambukizwa magonjwa kama: typhoid, cholera, minyoo, na kuhara damu.
Pia, iko hatari ya mioto hii ya holela barabarani kuunguza waendao kwa
miguu kandokando mwa barabara pamoja na kuunguza nyumba zilizo karibu na
majiko hayo. Hivi wizara ya afya inasubiri mabaya yawapate wananchi
ndiyo ichukuwe hatua?

True that, pokea ka like kangu ka kuandika.
 
Back
Top Bottom