Wizara ya Afya, muimulike na NHIF

Ng'azagala

JF-Expert Member
Jun 7, 2008
1,288
222
Ndugu Dr. Kigwangala kutokana na kwamba huwa unapita humu JF nakuandikia kuhusu kero za Bima ya afya NHIF kama zifuatazo ili usaidie kuzitatua

1. Gharama za matibabu hasa za vipimo na dawa huwa zipo “fixed” kiasi kwamba mgonjwa anaishia kupewa dawa dhaifu. Pia kuhusu vipimo – huwa kuna vipimo ambavyo mgonjwa analazimika kwenda kuomba kibali kwao
2. Hospitali chache zimesajiriwa na Bima, mf. Hospitali kubwa kama Aghakan ya Dar es Salaam na nyingine hakuna huduma ya NHIF
3. NHIF wameanza kuwekeza katika kujenga hospitali, na kuacha huduma zao bila kuziboresha. Ni nini “mission and vision” yao?

Kero ni nyingi – kama jingine la kucheleweshwa kwa kadi za uanachama nk. NHIF wanapaswa wafanye kazi kubwa kuboresha huduma zao ziendane na makato
 
Kwa Kuoengeza Tu.
Hii Sera Ya Huo Mfuko Kumchagulia Mwanachama Mnufaika Wameitoa Wapi? Anayejua Umuhimu Wa Mnufaika Ni Mwanachama Mchangiaji Na Sikumpangia Kama Ilivo Na Kuforce Eti Baba/mama Mkwe Nao, Wakati Mtu Anaweza Hata Kumchangia Rafiki Yake Na Si Lazima Circle Hyo Waloweka, Tumbua Hapo Mh Nwa
 
Kingine ni kukulazimisha kuweka watu wa kutibiwa wao badala ya kumpa mteja wao uhuru wa watu wa kutibiwa!!
 
kero ni nyingi muno, kwa watoto wanaozaliwa kwa sasa kuwasajili ni noma kwani wanasema tusubili marekebisho sasa yapata mwaka wanatibiwa nje ya hospitali wakati huduma hii tunakatwa, wakati mwingine ukipoteza kitambulisho kukipata noma sana,

huwezi kutumia barua ya police lost report ukatibiwa wakati evidence kuwa wewe ni mwanachama zipo, hapo nini maana ya system (yaani kuwa kwenye mfumo wa computer) mbona benki unaweza kutoa fedha kama umesahau kitambulisho ?

tutambue maana ya system. Kero nyingine ni kwamba, watu wa NHIF tunaibiwa sana na hospital binafsi unakuta kitu cha elfu 10 wanaweka 50 eti kwa kuwa wanachelweshwa kulipa , hii sio haki kabisa.

kero nyingine tunabaguliwa kupewa dawa, cha kujiuliza wanapeleka wapi hela zetu, nasikia ccm wamezikopa kwa ajiri ya uchaguzi sijui watarudisha lini.
 
Kati ya kero zangu kubwa ni huduma za NHIF. Unaenda hospitali unahudumiwa kama muhaini!!! Yaani kama kinyaa vile ukitoa CARD ya NHIF kwa wauguzi na madaktari. Why? Fedha mfano ninayolipia mie ni sawa na ama inazidi mchangiaji wa STRATEGIS ama TANESCO health fund, lakini kwa nini huduma nisipate hospital kama AGHA KHAN ya Dar es Salaam (Mwanza naambiwa AGHA KHAN wanaendelea kuwahudumia wanachama wa NHIF na hii yawezeekana kwa sababu ya uchache wa wanachama wenye GREEN CARD-na-assume hivyo) ama BOSCHI ya Kimara??? Regency, kwa wale tulio Dar es Salaam, ndipo palikuwa kimbilio letu, lakini hospital imezidiwa sana na sasa CARD ya NHIF inaonekana ni UCHURO!!!

Tunahitaji kufanya marekebisho ya sheria ili huu mfuko kma ilivyo mifuko mingine ya kijamii, mwanachama awe na uhuru wa kuamua ajiunge wapi. Wafanyakazi wa TANESCO ni watumishi wa UMMA lakini wana mfuko wao, similary watu wa BOT wanahudumiwa na STRATEGIS (niliwahi ona hili kwa mtumishi mmoja wa BOT) na wao pia ni watumishi wa UMMA. Kwa nini kwa watumishi wengine iwe LAZIMA ukiajiriwa tu, mkataba unasema utajiunga na NHIF??? Hili ni JIPU kubwa mno.

Wanachama wa NHIF kwa kweli hatupendezwi na huduma za mfuko katika kutupatia huduma za kiafya zenye staha na heshima. Mgonjwa hupona kutokana na tiba na huduma nzuri. Siyo karaha za manesi kisa tu kuwa mwanachama wa NHIF. Hatulazimishi sisis kuwa katika mfuko huu hivyo tusihukumiwe kwa kulazimishwa kwetu kuwa wanachama.

La mwisho ni kuwa ni kwa nini kuwa mwanachama wa mifuko miwili ya jamii kama mtumishi wa umma??? NSSF wanatoa fao la matibabu kwa wanachama wao mfano. Na huyo mwanachama anaweza kuwa ni mtumishi ambaye bado anachangia NHIF. Je, hakuna haja ya kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu wa jamii ambao utatakiwa kutoa fao la afya kwa wanachama wake maana kwa watumishi tunachangia kote kote mpaka kustaafu.

Hili liangaliwe jamani. Tunaumia na pia tunanyanyaswa na uanachama wa NHIF.
 
Mmeongea kweli tupu, itakuwa vizuri kama wahusika watafanyia kazi hizi kero. pia wauguzi wajaribu kuwathamini wanaotakiwa kupata huduma hiyo kupitia kadi hizo manake mmmh!
 
Mwanza kuna hospitali za CF na Kamanga ni nzuri lakini hazipokei NHIF cards. NHIF ni jipu pa ukweli.
 
huo ulazima wakujiunga na NHIF ukiwa mfanyakazi unatoka wapi, kwanini tusichague wenyewe mikataba ikafungwa popote?hivi hawa wanaotuchagulia watu wa kuwaweka wako sahii, kama mie nimerithiwa inakuwaje kwani hawa sio wazazi wangu wa kitovu.
 
Niliwahi kuona kuwa wameboresha bei za huduma zao kwa watoa huduma kwa wanachama kumbe, baadhi ya huduma zimepunguzwa gharama wakati vitu vinaendelea kupanda, nimeshangaa Sana hata hawaeleweki, watasababisha huduma kwa wanachama kuwa mbovu zaidi na kuwaona ni kero kwa watoa huduma.
 
Kati ya kero zangu kubwa ni huduma za NHIF. Unaenda hospitali unahudumiwa kama muhaini!!! Yaani kama kinyaa vile ukitoa CARD ya NHIF kwa wauguzi na madaktari. Why? Fedha mfano ninayolipia mie ni sawa na ama inazidi mchangiaji wa STRATEGIS ama TANESCO health fund, lakini kwa nini huduma nisipate hospital kama AGHA KHAN ya Dar es Salaam (Mwanza naambiwa AGHA KHAN wanaendelea kuwahudumia wanachama wa NHIF na hii yawezeekana kwa sababu ya uchache wa wanachama wenye GREEN CARD-na-assume hivyo) ama BOSCHI ya Kimara??? Regency, kwa wale tulio Dar es Salaam, ndipo palikuwa kimbilio letu, lakini hospital imezidiwa sana na sasa CARD ya NHIF inaonekana ni UCHURO!!!

Tunahitaji kufanya marekebisho ya sheria ili huu mfuko kma ilivyo mifuko mingine ya kijamii, mwanachama awe na uhuru wa kuamua ajiunge wapi. Wafanyakazi wa TANESCO ni watumishi wa UMMA lakini wana mfuko wao, similary watu wa BOT wanahudumiwa na STRATEGIS (niliwahi ona hili kwa mtumishi mmoja wa BOT) na wao pia ni watumishi wa UMMA. Kwa nini kwa watumishi wengine iwe LAZIMA ukiajiriwa tu, mkataba unasema utajiunga na NHIF??? Hili ni JIPU kubwa mno.

Wanachama wa NHIF kwa kweli hatupendezwi na huduma za mfuko katika kutupatia huduma za kiafya zenye staha na heshima. Mgonjwa hupona kutokana na tiba na huduma nzuri. Siyo karaha za manesi kisa tu kuwa mwanachama wa NHIF. Hatulazimishi sisis kuwa katika mfuko huu hivyo tusihukumiwe kwa kulazimishwa kwetu kuwa wanachama.

La mwisho ni kuwa ni kwa nini kuwa mwanachama wa mifuko miwili ya jamii kama mtumishi wa umma??? NSSF wanatoa fao la matibabu kwa wanachama wao mfano. Na huyo mwanachama anaweza kuwa ni mtumishi ambaye bado anachangia NHIF. Je, hakuna haja ya kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu wa jamii ambao utatakiwa kutoa fao la afya kwa wanachama wake maana kwa watumishi tunachangia kote kote mpaka kustaafu.

Hili liangaliwe jamani. Tunaumia na pia tunanyanyaswa na uanachama wa NHIF.

Ni sahihi mkuu ukiwa na kadi pale Regency ni mateso. Huduma utapata vizuri ila kutokana na uwingi wa watu na hivyo wametenga watu wa NHIF wanatibiwa tofauti ndiyo hiyo kero inakuwepo.
Ila wangeweza kusajiri hospitali kubwa nyingi Zaidi kama siyo zote na waweke utaratibu usio na usumbufu ili wanaotibiwa wasisubiri muda mrefu kupewa huduma. Wajifunze kwa mifuko mingine inafanyaje na kwanini wao iwe shida?
 
Eneo la afya linahitaji ewura yake coz madawa yanapanda/kupandishwa bei ovyo. Ukienda hospitali ukaona bei za zile dawa unazoandikiwa ni mungu mwenyewe anajua. Kuna wkt nilikuta dawa inauzwa elf 30 huku famasi za mtaani nikaona isiwe taabu kwa sababu nina bima ngoja niende na kadi hospitali nikapata dawa ileile niliyoiona kule mtaani kwa sh.elfu sabini!!
 
Mimi kero yangu kuhusu NHIF ni kwa upande wa upatikanaji wa vibali kwa baadhi ya dawa. Hii ni hasa kwa wagonjwa wa cancer. Ni mlolongo mrefu na wenye kuchosha mgonjwa. Mfano mgonjwa anatibiwa Bugando Hospital anaandikiwa dawa na daktari NHIF pale hospital wanamuandikia kibali cha kununua hiyo dawa ila inabidi uende mjini ofisi za NHIF upate kibali tena cha daktari wao hapo uwe umeshazunguka kwenye pharmacy zinazo-accept NHIF kujua dawa ulizoandikiwa zinapatikana wapi kwani hicho kibali kinajazwa jina specific la pharmacy , ukimaliza urudishe copy za hicho kibali hospital. Yaani imagine huyo ni mgonjwa siku nzima anatumia kuhangaika na wakati mwingine unakuta maduka yanayo-accept NHIF hayana hizo dawa hivyo inaweza kumchukua mgonjwa siku 2 hadi 3 akihangaika. Hapo ni kila mwezi mgonjwa anapoenda kuhudhuria clinic. Na wengine wanakuwa watoka nje ya mkoa ni kama adhabu.

Nadhani huu utaratibu sio mzuri, ingekuwa vema kama madaktari baada ya kujua mgonjwa atahitajika kutumia dawa kwa muda mrefu basi wa-recommend kwa NHIF kutoa kibali cha muda mrefu let say 4 or 6 months ili mgonjwa aweze kupata dawa za muda mrefu abakie tu ku- attend clinic kila mwezi.
 
Eneo la afya linahitaji ewura yake coz madawa yanapanda/kupandishwa bei ovyo. Ukienda hospitali ukaona bei za zile dawa unazoandikiwa ni mungu mwenyewe anajua. Kuna wkt nilikuta dawa inauzwa elf 30 huku famasi za mtaani nikaona isiwe taabu kwa sababu nina bima ngoja niende na kadi hospitali nikapata dawa ileile niliyoiona kule mtaani kwa sh.elfu sabini!!
NHIF ni mfuko kwa ajili ya kuwafaidisha watu fulani lakini sio kwa ajili ya kuwanuufaisha wanachama , mtu ukifika Hospitali Daktari na wauguzi wanakuona kama hauna maana yoyote na hata wakichukua sampuli ya damu au mkojo au vinginevyo havipimwi kabisa , wanabandika majibu wayatakayo na baadae mtu anapewa dawa akatumie bila ya hata kuwa na ugonjwa, ukitaka kujua fika hospitali ya Agakhani Dodoma yapo haya.
 
Kwa Kuoengeza Tu.
Hii Sera Ya Huo Mfuko Kumchagulia Mwanachama Mnufaika Wameitoa Wapi? Anayejua Umuhimu Wa Mnufaika Ni Mwanachama Mchangiaji Na Sikumpangia Kama Ilivo Na Kuforce Eti Baba/mama Mkwe Nao, Wakati Mtu Anaweza Hata Kumchangia Rafiki Yake Na Si Lazima Circle Hyo Waloweka, Tumbua Hapo Mh Nwa
Hata hapo mimi ndo nashangaa sana, na inashangaza kwa kweeli.Wataanzaje kumchagulia mtu wategemezi?? Hii Sheria ni mbaya sana kwa Wachangiiaji. Ila sishangai sana unaweza kuta lengo lao ni kuPata faida zaidi ya kutoa huduma,I think they are there for the Benefits.You know,Mwanachama akipewa Limit ya ni wakina nani wakujazwa, This automatically reduce number of his/her Dependant,hence few wategemeezi..POOR US....HONGERENI NHIF KWA KUTUNYIMA UHURU WA KUCHAGUA NA WAKATI HUO HUO MNATULA HELA ZETU
 
Back
Top Bottom