Kuna nyumba ya ibada hapa Mwenge Mpakani inalaza wagonjwa na kufanya vipimo vya MRI,CT Scan,X-ray, Ultra sound vya kienyeji. Bei ya vipimo hivi ni Tsh. 10,000/- kila kimoja,mgonjwa akipatikana na maradhi kutibiwa kwa kitu kinaitwa package ambayo ni kachupa ka asali ka ujazo wa ml 10 na bei ni kuanzia 70,000/- hadi 350,000/-.
Sina shida ghilba hii kwani ni ujinga wa hao wahanga wenyewe, ila tatizo ni mazingira ya kulaza wagonjwa hapo Wizara ya Afya inazo taarifa na kama ndiyo imeridhia uhuni huu?
View attachment 2830166