Wizara ya afya kwaweza kutokea mgororo mwingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya afya kwaweza kutokea mgororo mwingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maluluma, Mar 13, 2012.

 1. m

  maluluma Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Migogoro na migomo mingi huwa inasababishwa na kulea matatizo. Laiti matatizo yangekuwa yana tatuliwa maramoja yanapotokea migogoro ingepungua sana. Kuna taasisi moja katika wizara ambayo hivi karibuni kulikuwa na mgomo ule wa madaktari kuna matatizo makubwa sana ambayo kwa kiasi kikubwa yamelelewa na viongozi wa wizara. viongozi wa wizara wamekuwa wanafahamu kuhusu uozo wa taasisi hiyo lakini hawataki kushughulikia matatizo ya taasisi. Taasisi hiyo iliyo karibu na bahari inayohika na mambo ya misosi, mkuu wake ana scandali nyingi sana lakini viongozi wa wizara wamefumbia macho na kitu cha ajabu wanataka wampe mkataba aendelee tena kuongoza huku akiwa amestaafu. Mkuu huyo kapiga mkwara kuwa hawezi kuacha taasisi hatakama umri wa kustaafu umefika, ataendelea kuwa bosi bila kujali anatakiwa astaafu au la. Kisha sema mambo yote atanyosha yule mnene wa wizara ambaye alikuwa anang'ang'aniwa na madaktari ang'oke. Kwa kuendelea kumlea huyu bosi wa taasisi mnene wa wizara haoni anaweza kuzua mgomo mwingine. ukizuka mgomo huo tuseme ni bahati mbaya ihali bosi huyo anajulikana kwa tuhuma nzito alinazo: ufisadi, kachakachua mpaka mishahara ya wafanyakazi, anaendesha taasisi kama kioski chake na msululu wa mambo mengi sana. Lakini viongozi wa wizara wamenyamaza kuanzia yule mwana mama aliyeng'oka na sasa waziri mwenyewe. Huyu bwana kawaweka mfukoni. Hawawezi kumwajibisha. Hivi kwanini watu wapate mateso kwa kumkumbatia mtu mmoja wakati kuna watu wengi wenye uwezo na nia nzuri ya kuleta maendeleo wapo ?
   
 2. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Fitina, fitna, ftina, ftn
   
 3. kakakuona40

  kakakuona40 JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
Loading...