Wizara ya Afya kuungana na Polisi kukomesha ukahaba Dar

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuiunga mkono Polisi nchini katika operesheni ya kukamata wateja wa makahaba kuhakikisha biashara hiyo inakoma nchini.

Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu alisema takwimu zinaonesha wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa wa Ukimwi, ambapo kati ya Watanzania 100 wanaopimwa, sita ni wanawake na wanaume ni wanne pekee.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Dar es Salaam jana, Ummy alisema si haki kuwakamata wanawake wanaojiuza na kuwaacha wateja wao ambao ni wanaume.

“Ninalipongeza Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo kwa sababu imeonesha kutoegemea upande mmoja kwa kuwakamata wanawake makahaba. Wote wanaojiuza na wanaonunua huduma hiyo ni wakosaji wanaostahili kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tunaungana na Polisi kushiriki operesheni hiyo,” alisema. Alieleza kuwa, biashara ya ukahaba inayofanywa na wanawake isingekuwepo endapo wateja wasingekuwepo, hivyo, wateja wanastahili kukamatwa pia kwa sababu ndio wanaoichochea.

Ummy alisema familia nyingi zina misukosuko na wanawake wengi wamekuwa wakiteseka na wengine kuambukizwa magonjwa na waume zao wanaoshiriki biashara hiyo. Katika hatua nyingine, alisema sasa wanataka kuona idadi ya wanaume wateja wa biashara hiyo inatajwa sambamba na ya wanawake wanaokamatwa nao ili ndugu na wake zao wafahamu kuhusu tabia yao hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, alisema hatua ya kukamata wateja na wauza miili imetokana na makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Dar es Salaam.
 
HAPANAAAAAAAA kwa hili sikubaliani na serekali. Stress zetu tutazimalizia wapi?

Leave us alone!!
 
Hahaha! Dah sipati picha mtu mzima karibia kupata wajukuu anachorwa jina na picha kwa gazeti eti ni mteja wa chips funga! Kweli hii itapunguza hii tabia.

Nawashauri polisi na makachero wazungukie kwenye guest na lodge zote chocho za mjini pia. Kuna makahaba na vikahaba wanaishi humo kama nyumbani. Wanafanya biashara kwa mitandao ya kijamii na wateja wanawakuta humo na kumaliza kazi. Wasiishie barabarani tu na kwenye hizo regular bars&pubs..
 
Ndoto za mchana.
Machangu wapo hadi uarabuni ambako kuna sheria kali za uchangu sembuse bongo ncchi isiyo kidini.

yeye ummi kama ni mzanzibari hata kwao zenji machangu ni wa kumwaga.

Hakuna inchi ambayo hiyo huduma haipo na hakuna mahala unaweza kuiondoa.

Asitutafte ubaya,wanafanya mambo yao sisi tunawaangalia tu sasa naona wanaingilia anga zetu tutaua mtu.

Utuondolee take away alafu iweje, watu tuna stress zetu za kazini huko mnakaba hadi penalti alafu mje kutuondolea take aways zetu zinazotupa faraja baada ya matatizo mengi tunaua mtu.
 
Proffession ya kale zaidi duniani ni uchangu, ccm hawatoweza kuitokomeza kwa maigizo yao. Watafute mambo mengine ya msingi ya kuwanyia wananchi.
 
Machangudoa wapo mpaka maofisini mtawakamataje? au wanafikiri machangudoa ni wale waliopo barabarani peke yao. Na swala la kusema machangudoa wa barabarani au sehemu za starehe wanavunja ndoa na wana ukimwi si kweli. Wale machangudoa walioko maofini na kwenye vyuo ndiyo wanavyunja ndoa na ndiyo wenye ukimwi maana wenyewe wanajifanya hawajiuzi kumbe wanajiuza.
 
Ndoto za mchana.
Machangu wapo hadi uarabuni ambako kuna sheria kali za uchangu sembuse bongo ncchi isiyo kidini.

yeye ummi kama ni mzanzibari hata kwao zenji machangu ni wa kumwaga.

Hakuna inchi ambayo hiyo huduma haipo na hakuna mahala unaweza kuiondoa.

Asitutafte ubaya,wanafanya mambo yao sisi tunawaangalia tu sasa naona wanaingilia anga zetu tutaua mtu.

Utuondolee take away alafu iweje, watu tuna stress zetu za kazini huko mnakaba hadi penalti alafu mje kutuondolea take aways zetu zinazotupa faraja baada ya matatizo mengi tunaua mtu.
Aiseee kama vile nakuona unavyoandika kwa jazba pole sana mkuu itabid uwe unaagiza arusha manake hiyo operation Iko Dar tu . Huku arusha tunapeta .
 
Ndoto za alinacha hizo ni nchi gani duniani isiyokua na makahaba pamoja na kua na chumi na vipato vilivyoimarika kwa wananchi wake?vitu vingine ni kutafuta sifa tu yapo mambo mengi ya msingi bado hatujayakamilisha tunarukia makahaba?
 
Wizara ya afya inachangamoto nyingi kwa sasa kama kuboresha huduma za afya ikiwemo madaktari na vifaa na pia kuinua nidhamu ya watendaji wake.Hili la makahaba sidhani kama ni kipaumbele.Wateja wakuu wa makahaba ndio sisi tunaotunga na kuzisimamia sheria unadhani utaisha?
 
Kabla ya yote |Mh. Magufuli najua ulikuwa na nia nzuri saaaana za kupunguza wizara! Ninakushauri kabla Mawaziri hawajaanza kuchanganyikiwa kwa maana ya kutaka kugusa hapa na pale chonde gawanya hizi wizara ziwe mbili. Hizi wizara ni nyeti sana ( yaani moja iwe ya Afya na nyingine iwe Usatawishaji wa jamii ambayo ichanganywe na watoto, jinsia, walemavu na wazee) nasema hivi si kupinga hili suala la ukamataji lakini sina hakika kama ni la kipaumbele kuliko kukamata kina baba wanaotelekeza watoto wao mfano na tunakuwa na watoto wa mitaani. Ku-strenghen Ustawi wa jamii uweze shughulikia masuala ya kijamii., hii wizara ya pili ingejikita katika kuwacapacitate wanawake, watu wenye uwezoo midogo kwa kuwapa mikopo ha bei nafuu na elimu ya ujasiria mali. kwa mtazamo yangu haya mambo yataleta tija zaidi). Mi naona Wizara ya Afya yenyewe masuala yake yanatakiwa kuwa na Wizara inayojitegemea totally!
 
Tanzania hakuna sheria inayokataza ukahaba. Polisi wanawakamata makahaba na wateja wao kwa kutumia sheria ipi?
 
Biashara kongwe kabisa duniani haaa haaaa leo dada Ummy anataka kuikomesha tena kwa kuwatumia polisi,maana inaonyesha wazee wa kazi kwenye patrol nao wanajipoza kwa hao machangu
 
Hapo patamu.....Mzee Makamba alishindwa akasema wanaume wamemwangusha...kama unaenda kukamata na changudoa ni mteja wa boss utaweza?
Dawa ni kuwa na madanguro yalipe kodi kama ulaya tu. Acheni kupoteza muda na mali kwa kazi itakayowashinda
 
Kubwa ninaloliona ni kuwanufaisha polisi na posho zisizo rasmi huku biashara ikishamiri kidigitali zaidi.
 
Nadhani wangeanza kwanza na wamiliki wa Nyumba za kulala Machangudoa na Wageni ambazo kwa kiasi kikubwa zinamilikiwa na Wachagga
 
Nadhani wangeanza kwanza na wamiliki wa Nyumba za kulala Machangudoa na Wageni ambazo kwa kiasi kikubwa zinamilikiwa na Wachagga
na wa mabibo hostel je? manake hukawii kukuta vx asubuhi limeegeshwa.
 
Back
Top Bottom