Wizara inakaribisha Wadau kushiriki katika Shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara inakaribisha Wadau kushiriki katika Shughuli za Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo matamasha, ligi za michezo mbalimbali katika ngazi zote.

Mhe. Pindi Chana ametoa Rai hiyo Machi 31, 2023 jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau tofauti ambapo amesema kuwa Wizara yake inabariki shughuli zote zinazohusiana na Utamaduni, Sanaa na Michezo akiwataka kuzingatia taratibu Kanuni na miongozo mbalimbali iliyopo nchini.

Wadau hao ni Bw. Japhet Mswaki Mratibu wa Tamasha la Yakwetu Fair Festival, Bw. Rukemo Maasai Muaandaaji wa Tamasha la Maasai Festival pamoja na Bw. Fatih Karakus anayejihusisha na uibuaji wa vipaji vya michezo.

Aidha, Mhe. Balozi Pindi Chana amekutana na Waandaaji wa Tamasha la Pasaka mwaka huu wakiongozwa na Muimbaji wa nyimbo za Injili Christina Shusho ambalo amesema linalenga kuendelea kuhamasisha jamii kushirikiana na kukumbushana upendo Mila na Desturi za Kitanzania pamoja na kutoa burudani.

IMG-20230331-WA0056.jpg
IMG-20230331-WA0050.jpg
IMG-20230331-WA0054.jpg
IMG-20230331-WA0053.jpg
IMG-20230331-WA0052.jpg
IMG-20230331-WA0058.jpg
IMG-20230331-WA0059.jpg
IMG-20230331-WA0060.jpg
IMG-20230331-WA0064.jpg
IMG-20230331-WA0063.jpg
IMG-20230331-WA0061.jpg
 
Back
Top Bottom